The House of Favourite Newspapers

Tigo Ilivyozindua Wiki ya Huduma Kwa Wateja Utawapenda!

0

Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola (wapili kushoto) akizungumza. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji, Catherine Lutende, Kulia ni Msimamizi wa Huduma kwa Wateja, Henry Mboya na anayemfuatia ni Mwakilishi wa Watoa Huduma, Dora Mzinga.

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leo imezindua wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza leo Oktoba 5 mpaka 9, ambapo Mkuu wa Kitengo cha Huduma Kwa Wateja wa kampuni hiyo, Mwangaza Matotola amesema wataitumia wiki hii yote kufanyakazi karibu na wateja na watoa huduma wao ikiwemo kuwafikia walipo na kutatua changamoto wanazokutana nazo.

Mwakilishi wa watoa huduma, Dora Mzinga (kushoto) akizungumza.

Mwangaza amesema kampuni hiyo imezidi kuboresha mambo mbalimbali kwa wateja wake ikiwemo huduma ya kujirudishia muhamala ambao mteja aliutuma kimakosa kwa mtu mwingine.

“Tuna watoa huduma zaidi ya 1,000 nchi nzima ambao wanawahudumia wateja wetu na licha ya hivyo tumeongeza huduma za kidigitali za kuwawezesha wateja kujihudumia wenyewe kama vile kujirudishia muhamala alioutuma vibaya kwa mtu mwingine.

Mwangaza Matotola na Catherine Lutende wakijadiliana jambo kwenye uzinduzi huo.

“Kadili ulimwengu unavyokwenda na wakati nasi ndivyo tunavyojiboresha kila kukicha.

Hivyo basi wiki hii tutaitumia kuwafikia watoa huduma na wateja wetu waliopo sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujua changamoto zao ili nazo tuzitatue”. Katika kuonesha umahiri wa huduma zetu mwaka huu tumekuja na kauli mbiu iitwayo Dream Team ikimaanisha kikosi kazi chetu ambacho ni mabingwa wa kutoa huduma.

Watoa huduma wakiwa kazini.    

Naye Mwakilishi wa watoa huduma kwa wateja, Dora Mzinga akizungumza kwenye uzinduzi huo amesema wiki hii inawakumbusha watoa huduma kuongeza jitihada katika kutoa huduma kwa wateja ingawa siku zote wamekuwa wakitoa huduma bora.

Mmoja wa watoa huduma akiwa makini kwenye kitengo chake.

“Siku zote tumekuwa tukitoa huduma bora lakini wiki hii inatukumbusha kutoa huduma bora zaidi ya ile tunayotoa siku zote”. Alimaliza kusema Dora.

Mmoja wa wateja akiwapiga maswali maofisa wa Tigo.

Baada ya uzinduzi huo Msimamizi wa Huduma kwa Wateja Kituo cha Tigo, kilichopo Morocco, Henry Mboya aliwaonesha wanahabari na wateja jinsi watoa huduma wake wanavyofanya kazi ya kuwahudumia wateja ambapo wateja kadhaa waliokuwepo kwenye uzinduzi huo waliuliza maswali mbalimbali na kujibiwa.

Watoa huduma wakiwa kwenye pozi la picha baada ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply