The House of Favourite Newspapers

Tigo Yazindua Mtandao wa 3G Longido, Arusha

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Lilian Mwalongo hivi karibuni amezindua Mnara mpya ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G Longido mkoani Arusha. Uzinduzi huo umehudhuliwa na Mtendaji wa kijiji cha Longido Leiyo Laizer na Mwenyekiti wa kijiji Theresia Kashuma.

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kushoto) akiongea na wananchi wa Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mnara mpya ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G . Wa kwanza kulia ni Mtendaji wa kijiji cha Longido Leiyo Laizer na Mwenyekiti wa kijiji Theresia Kashuma
Mwenyekiti wa kijiji cha Longido Theresia Kashuma (kati kati) akiongea na wananchi wa Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mnara mpya wa Tigo ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G. Kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo na kulia ni Mtendaji wa kijiji cha Longido Leiyo Laizer
Meneja wa Tigo kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akipongezana na Mtendaji wa kijiji cha Longido Leiyo Laizer (kushoto) na mwenyekiti wa kijiji hicho Theresia Kashuma (kulia)muda mfupi baada ya kuzindua mnara mpya ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G
Maofisa wa Tigo wakiwahudmia wateja ambao ni wakazi wa Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mnara mpya ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G uliofanyika Longido jana.

Comments are closed.