The House of Favourite Newspapers

Tiko Adai Huu Mwaka Wa Kutoka

0

Tikoooooooo
Na Gladness Mallya

MSANII wa filamu Bongo, Tiko Hassan ameibuka na kudai baada ya mwaka jana kuwa mgumu kuliko kawaida kwake, anaamini wakati wake wa kutoka kimaisha sasa umefika.

Akipiga stori na gazeti hili, alisema mwaka huu atatimiza malengo yake yote, ikiwa ni pamoja na ndoto zake za kuwa msanii wa kimataifa na kuanzisha familia yake.

 “Mwaka huu kwa kweli sitakubali, nitatumia nguvu zangu zote hadi tone la mwisho kuhakikisha nafikia malengo yote niliyojiwekea kwa sababu ninajua hakuna linaloshindikana chini ya jua,” alisema.

 

Leave A Reply