The House of Favourite Newspapers

Rigwaride Ra afande-14

1

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:

“Bwana mimi naogopa peke yangu.”

“Hivi husikii wewe. Unadhani nani atakuja kujibanza hapa kwa maafande, hajipendi?”

Nikatoka hadi chooni. Ile nageuza kurudi ndani, yule afande mbaba naye anatoka kwake, akanishika mkono…

TAMBAA NAYO MWENYEWE…

“Wewe binti utakula jeuri yako. Nimesikia habari zako zote…kwa nini umefanya hivi lakini? Kama si mimi ungemjua afande Mwita wewe?”

“Bwana niache,” nilimwambia kwa sauti ya chini lakini yenye hasira…

“Sikuachi, wewe ni wangu, nikuachie nini sasa? twende kwangu…”

“Ha! Sitaki bwana.”

Alinishika kwa mabavu na kuniingiza chumbani kwake, akanikalisha kitandani…

“Kaa hapa!” aliniambia kwa ukali kidogo, nikakaa!

“Lakini sasa kule kwa afande Mwita kuna nguo zangu,” nilimwambia…

“Kachukue urudi hapa. Tena angalia asiamke. Wewe unaacha kuja kwetu wenye pesa unahangaika na afande mwenye mkopo kazini, atapata wapi pesa?” alisema yule afande mbaba.

Nilijikuta nasimama, nikatoka…

“Basi usifunge mlango,” nilimwambia. Moyoni niliamini niko sahihi kwa vile, afande huyo ndiye wa kwanza kuniona mimi, wengine ndiyo wakanitamani.

Yeye ndiye niliyekutana naye maeneo ya hospitali akiwa amekaa kwa msafisha viatu.

Basi, niliingia chumbani kwa afande Mwita, nikaweka shuka kitandani, nikavaa nguo zangu na kutoka polepole nikifunga mlango kwa machale sana.

Niliingia chumbani kwa afande yule mbaba. Chumba kilikuwa kimepoa. Afande alikaa kitandani akinisubiria kwa hamu kweli. Nilipoingia tu, akasimama na kwenda kufunga mlango na funguo, kachakacha, akanirudia na kunipandisha kitandani…

“Hapo sawa…hapo sawa,” alisema afande huyo kwa sauti iliyojaa uchu wa hali ya juu.

Tulikuwa wote kitandani sasa, joto la Dar usipime. Mlio wa feni ulitikisa chumba kizima…ziii…ziii!

Mara kwa mbali tukasikia mlango wa chumba kimoja wapo mle ndani ukifunguliwa…

“Afande Mwita huyo. Huo ndiyo mlango wake unavyolia,” alisema afande huyu mbaba.

“Haa! Atakuwa ananitafuta. Si ataingia kila chumba?” nilimuuliza…

“Hapana, ulipotoka kwenda kuchukua nguo zake na mimi nilitoka kwenda kufungua mlango wa uani nikauacha wazi…”

“Ili..?” nilimuuliza kwa kushangaa…

“Ili akitoka na kuukuta uko wazi ajue umeondoka zako.”

Niliachia tabasamu la kitandani. Niliamini kweli ni mbinu ya hali ya juu. Moyoni nikamsifu kwa ujanja huo.

Afande alitoka kitandani na kwenda kuzima feni haraka kisha akarudi…

“Huyu binti mjinga sana…inaonekana ni malaya tu… sasa anavyotoroka saa hizi akiuawa je? Mama yake si atanila nyama. Nikimkamata atanijua mimi ni nani?” tulimsikia afande Mwita akisema kwa kulalamika.

Tukacheka ndani kwa ndani, afande akanikumbatia na kunipa busu moja tu, zito!

Mara tukasikia mlango wa uani ukifungwa, mara tukasikia mlango wa chumbani kwa afande ukifungwa. Tukajua ameingia ndani kulala. Amesalimu amri…

“Lakini asubuhi nitatokaje mimi?” niliuliza.

“Nitajua mimi, wewe tulia.”

Kweli nilitulia. Afande akanishika na kunivutia kwake. Tukawa beneti, ziro distensi. Nikajua anataka nini. Mwee! Nilichoka lakini basi tu…

“Si tungelala kwanza baby,” nilimwomba…

“Wee! Utakula jeuri yako. Hapa hakuna kulala.”

“Plizi mpenzi wangu, kama hautajali naomba nilale kidogo ndipo nitakuwa huru kwa chchote utakachohitaji kutoka kwangu,” nilizidi kumwomba.

“Nasema hivi, utakula jeuri yako hapa hakuna kulala,” alisisitiza huku akiniangalia kwa macho ya uchu wa mapenzi.

Nilijua hata nikibisha vipi, hata nikiomba msamaha vipi, afande asingekubali. Lazima angetaka mpira uchezwe.

Na hii yote ilichangiwa na umbo langu kwani kwa mwanaume yeyote rijali, akiniona tu nilivyo hawezi kulala hata kama angetoka muda huohuo kucheza soka.

“Haya baba nakusikiliza,” nilimwambia.

“Wewe utakula jeuri yako, mimi siyo baba yako,” aliniambia na kunivutia mwilini mwake.

Sikuwa na la kufanya zaidi ya kujiachia kwa mbaba huyo mjeshi huku nafsi yangu ikiwa mbali kabisa na jambo alilotaka tulifanye kwani muda mfupi nilitoka kuchezeshwa ligwaride na afande Mwita tena kwa staili ya kusimama.

Basi, kwa tabutabu hivyo tuliingia uwanjani. Ushirikiano haukuwa wa kutosha kwangu, ila afande yeye alijitutumua mwenyewe mpaka mwishomwisho wakati anatangaza nia ndiyo na mimi nikapata nguvu ya kumsaidia kufika safari yake!!

Baada ya hapo tulilala zetu. Usingizi wenyewe kwangu ulikuwa wa maruweruwe.

Hali hiyo ilitokana na hofu niliyokuwanayo kufuatia kuwachanganya maafande wale kwa nyakati tofauti na kwenye jengo moja.

Niliwaza itakuwa vipi kama atafika saa kumi na mbili na kuambiwa na afande Mwita kwamba mimi nilitoroka usiku.

***

Nilikuja kushtuka kwenye saa kumi baada ya kuangalia saa ya kwenye simu yangu. Nikajisikia kwenda haja ndogo, nikamwamsha afande huyu mbaba…

“Nataka kwenda chooni.”

“Si unakujua?” aliniuliza.

“Ndiyo…”

“Nenda tu, mimi nakulinda.”

“Unanilinda wakati uko ndani?” nilimwuliza.

“Wewe nenda tu, usiwe na wasiwasi.

Nilitoka kitandani. Huyu bwana hakuwa na shuka, alikuwa akitumia blanketi. Na kwa joto la Dar blanketi hilo lilikuwa tu pembeni kwa kitanda limetulia.

Kwa hiyo ili kwenda chooni ikabidi nivae nguo zangu ndiyo nitoke. Nilivaa zote bwana!

Nikaenda chooni. Wakati natoka, afande alikuwa macho,  tena aliwasha taa kwa kutumia swichi ya kitandani, wenyewe mnaiita bed nini sijui..! nadhani ni bedi swichi!

Nikiwa chooni, nikasikia miguu ikitembea kuja usawa huo nikajua ni afande mbaba ameamua kunifuatulia.

Mara nikasikia ikiingia bafuni, nikasikia kukohoa. Mkohowo huo ulitaka kufanana na wa afande Mwira. Nikatulia kimya na kufuatilia ili nijue ni nani!

“Ee nivumiliee…nakupenda sana wewe…hata moyo wangu eee…” aliimba na ndipo nikajua ni nani sasa…

“Mh!” niliguna. Moyo ukaanza kwenda mbio. Nilijua nimeumbuka…

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Risasi Jumamosi ijayo.

1 Comment
  1. mahugila says

    Stick to only partiner!

Leave A Reply