The House of Favourite Newspapers

TikTok Yaikataa Microsoft, Yaungana na Oracle

0

 

WASHINGTON: Kampuni ya Marekani ya Oracle imeikataa Kampuni ya Microsoft na kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara (Business Partner) na kampuni ya China inayomiliki Mtandao wa TikTok, hii ni baada ya Rais Donald Trump kutaka Tiktok iuziwe Wamarekani la sivyo ataifunga isifanye kazi nchini humo.

 

Hata hivyo, haijafahamika iwapo ushirikiano huo wa TikTok na Oracle kama mshirika wa teknolojia unamaanisha kwamba Oracle itakuwa na hisa kubwa zaidi katika umiliki wa shughuli hiyo ya kimtandao.

 

Kampuni ya Microsoft ya Marekani ilikuwa inachukuliwa kama kampuni ya teknolojia ya Marekani yenye uwezo wa kununua shughuli za TikTok nchini Marekani kutoka katika kampuni-mama yake, ya ByteDance, na yenye uwezo mkubwa zaidi wa kushughulikia masuala ya usalama wa taifa, jambo lililosababisha uamuzi huo wa Trump.

Leave A Reply