TIMBWILI ZITO NJEMBA, DEMU WAZICHAPA BAADA YA KUTOKA GEST

MSICHANA na mvulana ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, mwishoni mwa wiki iliyopita walizua timbwili na kufunga mtaa kwa kizichapa kavukavu chanzo kikidaiwa ni kudhulumiana fedha.

 

Tukio hilo lililostaajabisha wengi lilitokea mida ya asubuhi maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo awali wawili hao walionekana wakitokea kwenye kiuchochoro, kabla ya kuanza kuzozana huku msichana akitaka apewe chake la sivyo patachimbika.

Demu huyo ambaye hakuweza kufahamika alikuwa akidai pesa kwa huduma gani aliyotoa, alionekana akihaha kupiga simu ambapo katika jitihada za mwanaume kuepusha shari, alisimamisha Bajaj ili waondoke eneo hilo.

Hata hivyo jitihada hizo ziligonga ukuta baada ya msichana huyo aliyekuwa amefura naye kuzama kwenye Bajaj hiyo na kuanza kumpa kashikashi mwanaume huyo akimtaka ampe pesa zake ndiyo aondoke. “Nipe pesa yangu ndiyo uondoke, sikubali nipe pesa yangu… na kwa nini ulitaka kunitoroka kule gesti, toa pesa yangu la sivyo hapa huondoki,” alisikika akisema msichana huyo hivyo kuwafanya watu wajue kumbe walitoka zao gesti.

 

Hata hivyo, wakati sekeseke likiendelea ndani ya Bajaj, demu huyo alitaka kumvutia kwa nje mwanaume huyo ili aweze kumtaiti ampe chake lakini njemba alikuwa ngangari hivyo Bajaj hiyo kuondoka eneo hilo kwa kasi wote wakiwa ndani. Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa mashuhuda ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Sneja alisema: “Inavyoonekana hawa wametokea gesti, wamepeana mambo sasa huenda jamaa alitaka kutoroka ndiyo likatokea hili timbwili.”

 


Loading...

Toa comment