The House of Favourite Newspapers

Timu ya Tanzania ya TSC Wanapata Chakula na Balozi Nchini Urusi

Timu ya Tanzania ya TSC wakiwa wanapata chakula cha jioni baada ya kualikwa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Simon Mumwi na maafisa na wafanyakazi wengine wa Ubalozi.

 

WATOTO wa Timu ya Tanzania ya TSC wakiwa wanapata chakula cha jioni baada ya kualikwa na  Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Simon Mumwi na maafisa na wafanyakazi wengine wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na viongozi wa timu na waratibu wa timu.

Timu hiyo ya watoto wa mitaani ya Tanzania kutoka kituo cha TSC cha Mwanza imeipata nafasi ya pili katika mashindano ya kombe la dunia la watoto wa mitaani nchini Urusi baada ya kupoteza mchezo wa fainali kwa 1-0 dhidi ya Brazil.

 

Timu hii ilionyesha mpira wa aina yake na imejitahidi sana tofauti na watu wengi walivyofikiria na kuona watoto wa mtaani hawaezi kufanya kitu. Lakini leo hii ndio wao katika soka wanaipa nchi heshima kimataifa.

Wao Wanarudi nyumbani wakiwa wameagwa na Mheshimiwa balozi wa Tanzania nchini Urusi na ubalozi kwa ujumla na kupewa heshima zote na nasaha kutoka kwa balozi huyo.

 

Pia watapokelewa kwa heshima na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. John Magufuli leo hii.

Kwa upande mwengine pia walipata nafasi ya heshima ya kuuliza swali lao kwa mchezaji wa Kimataifa wa Brazil na Arsenal aliekuja katika Fainali hio, Gilebrto Da Silva. Watoto hao walitunukiwa zawadi mbalimbali na kombe la mshindi wa pili.

Lakini Tanzania ikatoa kiungo bora wa mashindano hayo ambaye ni nahodha, Asteria Robert. Ikumbukwe kuwa timu hii imeruhusu mabao mawili tu kukwamishwa wavuni mwake na ndio timu pekee iliofungwa magoli machache katika mashindano. Timu hii imezifungwa timu kubwa kama Kazakhstan 1-0,Urusi 3-0 ,Marekani 5-0 na Uingereza 2-1.Tanzania imeendelea kuwa na heshima kubwa sana kwa Kombe la Dunia la watoto wa mitaani na timu ya watoto wa mitaani kuwa na rikodi nzuri kwani mwaka 2010 timu ya Tanzania ilifika nusu fainali huko Afrika na mwaka 2014 timu ya Tanzania ilikua bingwa huko Brazil.

 

Mashindano haya ya Street Child World Cup huandaliwa kila ikikaribia kombe la dunia la FIFA kila baada ya miaka 4 na nchi inayokuwa mwenyeji wa kombe hilo la FIFA na chini ya usimamizi wa shirika la Street Child United la Uingereza chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Mr. John Wroe.

Hongera na pongezi nyingi kwa watoto hawa. Wamefanya kazi kubwa sana. Wameonyesha mpira nzuri sana. Wameipa heshima nchi yetu na Afrika. Wanstahili sana kuwezeshwa na kuheshimiwa sana. Tuendelee kuwaunga mkono kama watanzania wafikie ndoto zao na wao pia ndio hazina ya Taifa katika soka letu.

Mohamed Mansour Nassor
SOYUZ Alumni Associaion of Tanzania.

Comments are closed.