The House of Favourite Newspapers

JUMA KASEJA AWATIBUA SIMBA TAIFA

KIPA wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania, Juma Kaseja ‘Tanzania One’ leo Jumamosi amewatibua Simba baada ya kuivuruga rekodi yao ya kutaka kumaliza Ligi Kuu ya VPL na kuchukua Ubingwa bila kupoteza mchezo baada ya kukamata penati Okwi na kuwafanya Kagera kutoka na ushindi wa bao 1-0 katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Kaseja amedaka penalti ya Okwi katika dakika za nyongeza hivyo Kagera Sugar kuvunja rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuwafunga Simba kwa msimu huu baada ya kupachika bao dakika ya 86 ya mchezo na kuibuka na pointi tatu  hivyo kujikusanyia jumla ya Pointi 34.

 

Awali kabla ya mchezo kuanza Nyota wa Kagera Sugar walisema kuwa licha ya kwamba wapinzani wao wameshatwaa Ubingwa, lakini watahakikisha wanashinda mchezo huo ili kuwatibulia sherehe yao jambo ambalo wamefanikiwa kulitimiza.

 

Timu ya Simba imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kuwa na alama 68 kwenye mechi 29 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC yenye alama 52 kwenye mechi 28 wala Yanga yenye alama 48 kwenye mechi 26.

Comments are closed.