The House of Favourite Newspapers

Tito Magoti Arudishwa Rumande – Video

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka Upande wa Mashitaka kutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusu upelelezi wa kesi inayomkabili Afisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Tito Magoti na mwenzake Theodory Gyan.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Upande wa Mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon na upande wa utetezi ukiwa na Wakili, Fulgence Massawe kuvutana juu ya matumizi sahihi ya maneno yanayotumika katika kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega.

 

Awali wakili wa Serikali, Wankyo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo upande wa utetezi umedai kesi hiyo ilipotajwa Februari 5, mwaka huu upande wa Mashitaka ulidai kesi hiyo ipo kwenye hatua nzuri.

 

Hata hivyo Hakimu anayendesha kesi hiyo ameahirisha shauri hilo hadi Machi 19, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

 

Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili Magoti na mwenzake ni kushiriki makosa ya kiuhalifu ya kumiliki programu ya Kompyuta iliyotengenezwa mahususi kufanya kosa la jinai na kuwawezesha kujipatia kiasi cha shilingi zaidi ya milioni kumi na saba.

Leave A Reply