The House of Favourite Newspapers

Tofauti Za Kisiasa Hazitaikomboa Z’bar

0

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ,Othman Masoud Othman amesisitiza umoja na mshikamano kwamba ndio njia kuu ya kuisadia Zanzibar kutoka hapa ilipo na kufikia malengo yake.

 

Ameyasema hayo jana Machi  05 katika Msikiti wa Masjid Arafa uliopo Mombasa Wilaya ya Magharib ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, alipoungana na waumini wa dini ya kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa.

 

Othman amesema”Rangi za vyama vyetu wala Itikadi za vyama vyetu vya siasa kwasasa sio suluhisho la ukombozi wa Zanzibar na badala yake tuwe wamoja na kuhakikisha tunajenga mapenzi na nchi yetu ili kuleta maendeleo, kwani maendeleo yakija kila Mwananchi atafaidika bila kuangalia itikadi yake”.

Katika kuendelea kusisitiza katika umoja  Othman amekumbushia ya kwamba; ” Mimi jukumu langu kubwa ni kumsaidia  Rais katika kutimiza ndoto ya maendeleo ambayo italetwa na umoja na mshikamano wa viongozi na Wananchi kwa pamoja na tukifanya hili itakuwa ni dua kubwa pia kwa kiongozi wetu Maalim Seif kwani hili aliliasisi na kulisimamia”.

 

Ameongeza kuwa  ni wazi kwamba katika kupigania hili na kufikia maendeleo kuna changamoto nyingi lakini Wananchi wakiwa wamoja na mshikamano basi nguvu itakuwa kubwa na mafanikio yatapatikana.

 

Aidha  amewataka waumini hao kujua ya kwamba ili kiongozi afanye kazi zake na mambo kwenda vizuri basi ni lazima na waongozwa (Wananchi) wawe tayari na wawe wema kama wema wanaoutafuta kwa kiongozi wao.

Baada ya Ibada hiyo Makamu wa Rais  Othman alifika nyumbani kwa marehemu Maalim Seif kwa lengo la kukutana na kutoa mkono wa pole kwa wana familia wakiongozwa na Mama Awena, Mke wa Marehemu Maalim Seif.

Leave A Reply