The House of Favourite Newspapers

Tonombe, Tuisila Wamaliza Usajili wa Mcongo Yanga

0

IMEELEZWA kuwa viungo raia w DR Congo, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ndiyo wamefanikisha usajili wa beki wa AS Vita, Shaaban Djuma.Tetesi za usajili zinasema kuwa beki huyo tayari amekamilisha usajili wake kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

Beki huyo raia wa Congo, atajiunga na Yanga kama mchezaji huru baada ya mkataba wake wa kuendelea kukipiga Vita kumalizika, hivyo anaruhusiwa kujiunga na klabu hiyo.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, beki huyo tayari amesaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Yanga baada ya kufikia muafaka mzuri.Mtoa taarifa huyo alisema kuwa usajili wa beki huyo umefanikishwa na Wacongo wenzake Tonombe na Kisinda ambao ndio walitumia nguvu nyingi kumshawishi nyota huyo kusaini Yanga.

Aliongeza kuwa beki huyo anatarajiwa kujiunga na Yanga mapema mwanzoni mwa Julai, mwaka huu tayari kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

 

“Kama unakumbuka vizuri, Simba ndiyo walikuwa wakimfuata Djuma kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ambayo yalishindwa kufikia muafaka mzuri ya yeye kusaini mkataba.“Wakati Simba wakipambania kuwania saini ya beki huyo, ndiyo viongozi wa Yanga waliwatumia baadhi ya viongozi wa AS Vita kwa ajili ya kumshawishi asaini Yanga.

 

“Tofauti na viongozi pia wachezaji wa Yanga, Wacongo wenzake ambao ni Kisinda na Mukoko walishiriki kwa asilimia kubwa kumshawishi ili ajiunge na Yanga, hivyo akakubali na kusaini kwa siri miaka miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mshauri wa Yanga, raia wa Afrika Kusini, Senzo Mazingisa, hivi karibuni alisema: “Tayari tumekamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji na katika hili la usajili, tumekuwa tukifanya kwa usiri mkubwa.“Kikubwa hatutaki kuingiliana katika usajili na timu pinzani kwa kuhakikisha tunawasajili wachezaji wote walio kwenye mipango yetu.”

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

 

Leave A Reply