TOP 8 MISS AFRICA 2018

Image result for THULISA KEYI (SOUTH AFRICA)

  1. THULISA KEYI (SOUTH AFRIKA)

Thulisa Keyi huyu ndiye namba moja kwenye lisiti hii. Ni mrembo aliyeshinda kinyang’anyiro hicho kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Mei kwenye Ukumbi wa Sun Arena katika Jengo la Time Square, Pretoria na Bonang Matheba ndiye alikuwa ‘host’ wakati Thulisa akiwaburuza warembo 28.

MASHINDANO ya Miss World mwaka huu yatakuwa ni ya 68 kufanyika tangu kuanzishwa kwake na yatafanyika jijini Sanya, nchini China, ambapo Miss kutoka India, Manushi Chhillar atakuwa anakapidhi taji hilo kwa Miss World mpya.  Katika mashindano ya mwaka huu yatakayofanyika Desemba 8; hadi juzi (Jumatano), nchi shiriki takriban 85 zilikuwa zimekwisha pata washiriki wake. Yapata nchi 25, zinasubiriwa kupeleka majina ya washiriki mpaka ifikapo Oktoba 8, mwaka huu. Sasa kwa upande wa Afrika, hawa ni washiriki 8 bora, watakaotuwakilisha kwenye kinyang’anyiro hicho cha kukata na shoka.Image may contain: 1 person, smiling, standing

  1. MUSA KALALUKA (ZAMBIA)

Mrembo kutoka Lusaka, Musa Kalaluka ndiye ataiwakilisha Zambia kwenye mashindano ya Miss Dunia 2018 huko China. Mrembo huyu aliwabwaga warembo 12 tu walioshiriki katika kumsaka mlimbwende wa nchi hiyo!

  1. TIWONGE MUNTHALI (MALAWI)

Kinyang’anyiro cha kumpata Miss Malawi 2018, kilifanyika Jumamosi iliyopita kama ilivyo kwa Tanzania, mrembo kutoka Jiji la Lilongwe, aitwaye Tiwonge Muntali ndiye aliibuka kidedea miongoni mwa warembo 14.Image result for BELINDA POTTS (ZIMBABWE)

  1. BELINDA POTTS (ZIMBWABWE)

Shindano la kumsaka mrembo wa Zimbwabwe 2018, kilifanyika Jumamosi iliyopita kama ilivyo kwa Tanzania, Malawi na nchi nyingine ambazo ziligonganisha tarehe ya shindano hilo. Mrembo mwenye miaka 21, Belinda Potts ndiye aliibuka mshindi akiwaburuza warembo wenzake 14!Image result for iradukunda liliane miss rwanda 2018

  1. LILIANE IRADUKUNDA (RWANDA)

Shindano la Miss Rwanda 2018 lilifanyika mapema sana mwaka huu. Ilikuwa ni mwezi Februari ambapo Liliane Iradukunda aliibuka mshindi akichukua nafasi ya nduguye Elsa Iradukunda, aliyekuwa Miss Rwanda mwaka uliopita. Liliane aliibuka mshindi akiwagalagaza wasichana wenzake 20.Image result for MISS TANZANIA 2018

  1. QUEENELIZABETH MAKUNE (TANZANIA)

Kwa upande wa hapa nyumbani, Queenelizabeth kutoka Dar es Salaam, ambaye ni mshindi wa Miss Kinondoni mwaka huu ndiye ataiwakilisha Tanzania huko China kwenye Miss World. Mrembo huyu ataelekea China na Bendera ya Taifa akiwa amewaburuza warembo 20.Image result for QUIIN ABENAKYO (UGANDA)

  1. QUIIN ABENAKYO (UGANDA)

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ndiye alikuwa jaji mkuu kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Uganda 2018, kilichofanyikia jijini Kampala mwezi uliopita. Mshindi katika shindano hilo alikuwa Quiin Abenakyo, mrembo mwenye miaka 22, aliyefanikiwa kuwashinda warembo 21 waoshiriki wakitoka majiji mbalimbali ya taifa hilo.Image result for FINALI GALAIYA (KENYA)

  1. FINALI GALAIYA (KENYA)

Kwa upande wa Kenya, kinyang’anyiro cha mamiss kilifanyika pia siku ya Jumamosi iliyopita huko Westlands, Nairobi ambapo Finali Galaiya mshindi wa Miss India Kenya mwaka (2016), ndiye aliyeibuka mshindi wa kinyang’anyiro cha Miss Kenya 2018. Finali alikuwa kidedea kati ya warembo 26; ndiye anachukua namba mbili kwenye listi hii.

 

Loading...

Toa comment