The House of Favourite Newspapers

Top ten: Mastaa waliowaua wapenzi wao!

0

Earl-Hayes-and-VH1-Star-Stephanie-Moseley

Earl Hayes alifanya tukio lililoacha watu midomo wazi, alipomuua kwa kumpiga risasi mkewe, Stephanie Mosley pichani.

Makala: SIFAEL PAUL na Mtandao

Baadhi yetu tumesikia au kusoma juu ya watu wa kawaida, maarufu na mastaa mbalimbali duniani kukutana na mikasa ya kutisha na wakati mwingine kugharimu uhai wao. Lakini wapo baadhi ya mastaa waliokwenda mbele zaidi na kujikuta wakiwaua watu wao wa karibu wakiwemo ndugu, wapenzi, wachumba na wake au waume zao.
Leo kwenye ukurasa huu tunakuletea mastaa kumi (10) duniani walioacha historia kwa kuwaua wapenzi wao na baadhi yao kujiua;

Oscar Pistorius (R) and his girlfriend Reeva Steenkamp pose for a picture in Johannesburg, February 7, 2013. South African "Blade Runner" Oscar Pistorius, a double amputee who became one of the biggest names in world athletics, was charged on February 14, with shooting dead his girlfriend at his home in Pretoria. Picture taken February 7, 2013. REUTERS/Thembani Makhubele (SOUTH AFRICA - Tags: CRIME LAW SPORT ATHLETICS TPX IMAGES OF THE DAY) - RTR3DS4U
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius alidaiwa kumuua mchumba’ke, Reeva Steenkamp (aliyekuwa modo maarufu) akiwa naye katika picha.

 

10: CHRIS BENOIT
Chris Benoit alikuwa mwanamasumbwi wa Canada ambaye alipata ustaa mkubwa wakati wa kipindi chake kabla ya majanga. Ilikuwa nyumbani kwake, Georgia nchini Marekani, Juni 22, 2007, alipoibua mshtuko mkubwa baada ya kumuua mkewe na mwanaye wa kiume. Siku mbili baadaye naye alijiua kwa kujinyonga nyumbani kwake. Baadaye ilielezwa kuwa chanzo kilikuwa ni wivu wa kimapenzi.

Jovan-Belcher-Kasandra-Perkins-and-Daughter

Mwanasoka wa Marekani, Jovan Belcher akiwa na Kasandra Perkins.

9: EARL HAYES
Mwaka 2014, Rapa wa Marekani, Earl Hayes alifanya tukio lililoacha watu midomo wazi, alipomuua kwa kumpiga risasi mkewe, Stephanie Mosley wakiwa kwenye ‘apatimenti’ ghorofani akimtuhumu kwa usaliti kisha naye kujiua. Stephanie Mosley alikuwa ni bonge la mcheza shoo.

8: ROBERT BLAKE
Mwaka 2001, mwigizaji wa Marekani, Robert Blake alidaiwa kumuua mkewe wa pili, Bonnie Lee Bakley. Miaka minne baadaye, Novemba, 2005, alipatikana na hatia ya kufanya mauaji hayo lakini chanzo cha tukio hilo hakikuwekwa wazi.

Michael-Jace-and-Wife-April-Jace

Mwigizaji mwingine wa Marekani, Michael Jace akiwa na April Jace.

7: MICHAEL JACE
Mwigizaji mwingine wa Marekani, Michael Jace ambaye alikuwa kinara wa maigizo ya The Shield, mnamo Mei 19, 2014 alikiri kumuua mkewe, April Jace huku akiacha maswali kwa mashabiki wake kwa kuwa alikuwa na utajiri mzuri. Chanzo cha mauaji hayo kilifanywa siri ya kifamilia.

6: RUSSELL NEAL
Mwanamuziki wa R&B wa Marekani, Russell Neal, akiwa na singo yake maarufu ya I Like the Way, mwaka 2014 alikwenda mwenyewe polisi kuripoti kifo cha mkewe ndipo akakamatwa baada ya mwili wa mkewe kukutwa na majeraha ya kipigo.

Robert-Blake-and-Bonnie-Lee-Bakley

Mwigizaji wa Marekani, Robert Blake alidaiwa kumuua mkewe wa pili, Bonnie Lee Bakley.

5. RAE CARRUTH
Mwanasoka maarufu wa Marekani, Rae Carruth, mwaka 1999 alidaiwa kuzuia gari la mchumba’ke aliyekuwa mjamzito ambapo walitokea watu na kumuua mwanadada huyo. Baadaye iliripotiwa kwamba, jamaa huyo ndiye aliyekodi wauaji wafanye kazi hiyo kisa kikidaiwa ni usaliti. Carruth anatumikia kifungo jela akitarajiwa kuachiwa huru Oktoba 22, 2018.

4. OSCAR PISTORIUS
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius alidaiwa kumuua mchumba’ke, Reeva Steenkamp (aliyekuwa modo maarufu) wakiwa nyumbani huko Pretoria nchini Afrika Kusini. Ilikuwa Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day, Februari 14) mwaka 2013. Pistorius, katika maelezo yake alisema kuwa alidhani wamevamiwa na majambazi ndipo akafyatua risasi na kujikuta akimuua mchumba’ke huyo.

Gig-YoungMwigizaji wa Marekani ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya Academy, Gig Young.

3. JOVAN BELCHER
Mwanasoka wa Marekani, Jovan Belcher, mwaka 2012 alisababisha sintofahamu baada ya kudaiwa kumuua aliyekuwa mchumba’ke wa kitambo, Kasandra Perkins baada ya mabishano makali ya kimahusiano.
Aliondoka nyumbani na kwenda mbali na kwake kisha akajiua kwa kujipiga risasi kichwani huku wakiacha mtoto yatima wa kike.
2. O.J SIMPSON
Mwigizaji, mwanasoka na mtangazaji wa Marekani, Orenthal James ‘O.J’ aliyekuwa maarufu miaka ya 90, anaaminika ndiye aliyemuua mkewe na rafiki yake. Pamoja na kwamba wakili wake aliendelea kumtetea kuwa hakufanya mauaji hao, lakini bado watu waliamini yeye ndiye aliyefanikisha tukio hilo.
1. GIG YOUNG
Mwigizaji wa Marekani ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya Academy, Gig Young alioa mara tano ambapo alidaiwa kumuua mkewe wa tano ikiwa zimepita wiki tatu tu tangu alipofunga naye ndoa. Baadaye Gig alijiua kutokana na matatizo binafsi ambapo hadi leo hakuna mwenye maelezo ya sababu hasa iliyosababisha amuue mkewe na yeye kujiua.

Leave A Reply