The House of Favourite Newspapers

TRA Yakusanya Tril. 11, Julai-Desemba

0

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema katika kipindi cha Mwezi Desemba 2021 imekusanya TZS trilioni 2.51 kati ya lengo la kukusanya Tsh. Trilioni 2.29, makusanyo hayo yana ufanisi wa 109% na ndicho kiwango cha juu kukusanya kwa mwezi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mwaka 1996.

 

Katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2021/22 (Julai – Desemba 2021, TRA imekusanya TSh. trilioni 11.11, sawa 98% ya lengo la makusanyo ya Tsh. Trilioni 11.302.

 

Katika taarifa yake, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata amesema “kwa namna ya pekee Mamlaka inapenda kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa miongozo aliyoitoa kwa Mamlaka.

Leave A Reply