The House of Favourite Newspapers

Transfoma Tano Kuwasha Umeme Muriet Arusha – Video

0

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Makao Makuu, limekabidhi transformer kwa kata ya Muriet jijini Arusha kwa ajili ya kuwasha umeme kwa wakazi wa vijiji vya kata hiyo.

Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo ameonesha furaha yake baada ya kupata transformer hiyo ambayo ni miongoni mwa transformer tano zitakazowasha umeme katika Kata ya Muriet.

“Leo tumekabidhi transformer kwa ajili ya Mitaa ya Nado kusini, Eliwanyi, Embalaruwai kwenye Kata ya Muriet. Eneo hili zinatakiwa transformer 5 na zote zipo tayari. Asanteni Wizara ya Nishati na Tanesco. Shukran kwa Rais Samia!”

Leave A Reply