Trump Aapa Kulipiza ‘Mara 1,000’ Shambulio la Iran

 

RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameapa kwamba shambulio lolote litakalofanywa na Iran litajibiwa mara 1,000 kwa ukubwa, baada ya ripoti kuwa Iran inapanga kulipiza kisasi baada ya kuuawa kwa jenerali wa ngazi ya juu, Qasem Soleimani.

 

Ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani, zimenukuu maafisa ambao hawakutajwa majina, wakisema kuwa mpango unaodaiwa kupangwa na Iran wa kumuua balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini ulipangwa kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

 

“Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Iran inaweza kuwa inapanga mauaji hayo, ama mashambulizi mengine, dhidi ya Marekani kwa kulipiza kisasi cha kuuawa kwa Soleimani,” Trump aliandika katika ukurasa wa Twitter.

 

Amesema shambulio lolote litakalofanywa na Iran, kwa njia yoyote ile, dhidi ya Marekani litajibiwa kwa shambulio kubwa zaidi ambalo litakuwa mara 1,000 zaidi kwa ukubwa.

 
Toa comment