The House of Favourite Newspapers

Trump Ajisalimisha Mahakamani, Anakuwa Rais Wa Kwanza Marekani Kushitakiwa! (Picha +Video)

0
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump (katikati) akipungia mkono umati baada ya kuingia ndani ya Mahakama na alijisalimisha.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekana mashtaka baada ya kushtakiwa kwa makosa 34 ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na kughushi rekodi za biashara.

Donald Trump ameondoka kwenye chumba cha mahakama huko Manhattan.Hakutoa maoni yoyote na kupuuza maswali kutoka kwa waandishi wa habari. Trump atarejea nyumbani kwake Florida, ambako inatarajiwa atazungumza baadaye.

Ilichukua dakika chache kwa msafara wa rais huyo wa zamani kusafiri umbali wa kilomita 6.4 (maili 4) kwa gari kutoka nyumbani kwake huko Trump Tower hadi Mahakama ya Jinai ya Manhattan. Wakati wa safari hiyo, alichapisha kwenye mtandao wa kijamii: “Inaonekana ajabu — WOW, watakuja KUNIKAMATA”.

Alionekana mtulivu alipokuwa akiingia ndani ya mahakama, akisimama kuupungia mkono umati.
Baada ya kuingia ndani, alijisalimisha kwa mamlaka na kuandikishwa na kushughulikiwa. Kisha alionekana akiingia kwenye chumba cha mahakama.

Leave A Reply