The House of Favourite Newspapers

Mbunge Shigongo Amshukuru Rais Samia Kuchimba Visima Buchosa- Video

0

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amekutana na kufanya kikao na wananchi wa kitongoji cha Nyangalamila ambao siku chache zilizopita waliandamana wakipinga kitendo cha diwani wa eneo hilo kufukia kisima walichokuwa wanachimba.

Katika kikao hicho, Shigongo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa kuamua kuondoa tatizo la maji kwa kupeleka wataalamu wa kupima na kuchimba visima virefu Ili kuondoa tatizo la maji katika eneo hilo na kuepusha vifo vinavyotokana na watu kuliwa na mamba wakienda kuchota maji ziwani.

Leave A Reply