The House of Favourite Newspapers

Trump Alilaumu Kundi la ‘ANTIFA’ Kwa Mashambulizi Bungeni

0

RAIS wa Marekani, Donald Trump, anaamini kinafiki kwamba kundi la wapinga ufashist lenye mrengo wa kushoto (ANTIFA) lilihusika katika mashambulizi ya Jumatano wiki iliyopita Bungeni (Congress), lakini  hakubali lawama kwa tukio hilo lililosababisha vifo vya watu watano.

 

Kevin McCarthy, kiongozi wa wawakilishi rasmi wachache bungeni  aliwaambia wafuasi wa chama cha Republican jana kwamba Trump anastahili lawama kwa shambulio hilo na amekubali kuwajibika, kwa mujibu wa vyanzo vya watu wanne wa chama hicho.

 

Kevin McCarthy (kushoto) akiwa na Rais Donald Trump, Februari 2020.

Hata hivyo, Trump jana alitangaza hali ya hatari jijini Washington DC kukiwa na wasiwasi pia kwamba hilo linaweza kuathiri kuapishwa na rais mteule, Joe Biden.

 

Tangazo hilo linatoa kibali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Shirikisho kuhusu masuala ya dharura, kuwasiliana na serikali za mitaa za sehemu husika kama chama cha Democrats kinavyotaka.

 

Wiki iliyopita vurugu zilisababisha vifo vya waandamanaji wanne mitaani na ofisa mmoja wa polisi, ambapo watu wengi walijeruhiwa na nyumba nyingi kuporwa vitu na mali mbalimbali.

 

 

 

Leave A Reply