The House of Favourite Newspapers

Trump Amfuta Kazi Mkuu wa Usalama wa Uchaguzi

0

RAIS Donald Trump wa Marekani  amesema “amemfuta kazi ” mkuu wa usalama wa mtandao na shirika la usalama na miundombinu ya uchaguzi (Cisa), Chris Krebs, kwa taarifa zake “zisizo sahihi kwa kiwango cha juu ” kuhusu maadili ya kura.

 

Wiki iliyopita Trump alimfuta kazi waziri wa ulinzi, Mark Esper, huku kukiwa na ripoti kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya utiifu wa mkuu huyo wa Pentagon.

 

Kuna tetesi mjini Washington DC kwamba kabla ya Trump kuondoka madarakani mwezi Januari, Mkuu wa CIA, Gina Haspel, na mkurugeni wa FBI, Christopher Wray, huenda wakawa miongoni mwa wale watakaofutwa kazi na Trump.

 

Anaripotiwa  kutoridhishwa kwa Ikulu ya White kuhusu tovuti  kuhusiana na ule unaoitwa udhibiti wa taarifa za tetesi- Rumor Control, ambao ulipinga taarifa za upotoshaji, ambazo nyingi zilitumwa  na rais mwenyewe.

 

Maafisa wa uchaguzi wanasema kura ya mwaka huu ilikuwa “moja ya kura salama zaidi ” katika historia ya Marekani.

Taarifa za Reuters zinasema kuwa White House haikufurahishwa hasa na ujumbe wake wa mtandao ambao ulipinga dhana potofu uliodai kwamba kuna kompyuta maalumu za kiintelijensia zilizotumika kuhesabu kura zinazofahamika kama Hammer na Scorecard ambazo ziliingilia na kuvuruga hesabu ya kura za taifa.

 

Muda mfupi kabla ya kufutwa kazi, alituma tweet iliyoonekana kuyalenga madai ya Trump kwamba mashine za kupigia kura katika majimbo kadhaa zilibadilisha kura zake na kuzipeleka kwa hasimu wake Joe Biden.

 

Leave A Reply