The House of Favourite Newspapers

Trump na Kampuni Yake Watuhumiwa kwa Kusema Uongo Kuhusu Utajiri Wake

0
Rais wa zamani Donald Trump

Wakati baadhi ya biashara zake za majumba yenye thamani kubwa zaidi zikiwa mashakani, Rais wa zamani Donald Trump anasema atafanya safari adimu kwa hiari yake huko New York kwa ajili ya kuanza kwa kesi ambayo tayari imepelekea kwa maamuzi ya jaji kwamba alitenda ulaghai katika biashara zake.

“Nitakwenda Mahakamani kesho asubuhi kupigania jina langu na heshima yangu,” Trump aliandika Jumapili usiku katika mtandao wake wa Truth Social.

Trump alipiga kelele katika ujumbe wake alioubandika kwa Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James, ambaye amemfungulia mashtaka, na Jaji Arthur Engoron, ambaye anasikiliza kesi isiyokuwa na jopo la mahakama na kufanya maamuzi ya ulaghai wiki iliyopita.

“Hii KESI YOTE NI UONGO!!!” Trump aliandika. “Nitakutana nanyi Mahakamani – Jumatatu Asubuhi.”

Kesi hii ni kilele cha uchunguzi uliofanywa miaka mingi na James, ambaye amemtuhumu Trump na kampuni yake kwa kawaida ya kusema uongo kuhusu utajiri wake katika nyaraka za mahesabu.

Wiki iliyopita, Engoron alikamilisha madai ya juu kwa kesi hiyo kabla ya hata kuanza kusikilizwa, akitoa uamuzi kuwa Trump alikuwa na kawaida ya kudanganya mabenki, makampuni ya bima na wengine kwa kuongeza thamani ya mali zake katika makaratasi yanayotumika kufikia makubaliano na kujipatia mikopo.

Rais wa zamani huyo na nani ni nani kati ya watu walioko katika mtandao wake – watoto wake wawili wa kiume, watendaji wa Taasisi ya Trump na wakili wake wa zamani ambaye amegeuka kuwa adui yake Michael Cohen wameorodheshwa kati ya darzeni ambao wana uwezekano wa kuwa mashahidi.

Trump hatarajiwi kutoa ushahidi kwa wiki kadhaa. Safari yake ya kwenda mahakamani Jumatatu itakuwa ni safari ya kipekee kutokana na uzoefu wake wa huko nyuma.

Trump hakufika mahakamani kama shahidi au msikilizaji wakati kampuni yake na mmoja wa watendaji wake wa juu alipokutwa na makosa ya ulaghai wa kodi mwaka jana.

Hakuhudhuria, iwe, kwa ajili ya kesi mapema mwaka huu ambapo jopo la mahakama lilimkuta na kosa la kumshambulia kingono mwandishi E. Jean Carroll katika chumba cha kubadilisha nguo kwenye duka la nguo.

Kwa namna Fulani, hata hivyo, kesi hii mpya inakuja na gharama kubwa zaidi.

James, Mdemokrat, anataka alipishwe faini ya dola za Marekani milioni 250 na kupigwa marufuku kufanya biashara mjini New York.

Uamuzi wa Engoron alioutoa wiki iliyopita, iwapo utakubaliwa katika rufaa, utahamisha udhibiti wa baadhi ya makampuni yake kwa msimamizi atakaye chaguliwa na mahakama na inawezekana akamlazimisha kuachia mali zake zenye thamani kama vile Trump Tower, Jengo la ofisi za Wall Street, eneo la mafunzo ya mchezo wa golf na biashara katika kitongoji.

Trump aliita hilo kuwa” ni adhabu ya kifo kwa kampuni.”

UKWELI WOTE WARDA KUDAIWA KUONEKANA AFRIKA KUSINI, MAZITO YAIBUKA TENA | MAPITO

Leave A Reply