The House of Favourite Newspapers

Trump, Xi Jinping Wakubaliana Kusitisha Uhasama Kibiashara

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesifia mazungumzo kati yake na Rais wa China, Xi Jinping na kuyataja kuwa mazuri kuliko yalivyotarajiwa.

Sambamba na hilo, Trump ameahidi kusitisha kuongeza ushuru kwa bidhaa za China wakati mazungumzo kati yao yakiendelea.

Kama kawaida yake, Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, akieleza kuwa ubora wa mazungumzo ni muhimu zaidi kwake kuliko kasi.

Mazungumzo ya wawili hao yalifanyika Jumamosi mjini Osaka Japan pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa G20, ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi.

Vilevile Trump na Xi walikubaliana kuendelea na mazungumzo ya kusitisha uhasama wa kibiashara kati ya nchi zao.
Marekani na China zimekuwa kwenye mzozo wa kibiashara huku pande zote zikiongeza ushuru kwa bidhaa zinazotoka kwa mwenzake.

 

Comments are closed.