The House of Favourite Newspapers

MAN UTD WAKUBALI YAISHE KWA POGBA

Paul Pogba

MANCHESTER United wamekubali yaishe kwa Paul Pogba, ambapo wameamua kuweka hadharani bei yake. Klabu hiyo inaaminika imechukua hatua huyo kufuatia Pogba mwenyewe kuonyesha nia ya kutaka kuondoka baada ya kudai anataka kutafuta changamoto mpya kwingineko.

 

Pia kuna taarifa kuwa Pogba mwenyewe amewasiliana na kocha mpya wa Juventus, Maurizio Sarri kumwomba amsajili katika kikosi chake cha msimu ujao wa 2019/20. Pamoja na shinikizo la Pogba lakini klabu kama Real Madrid ilikuwa inawapa presha kubwa ya kumtaka staa huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Kufuatia maombi ya Pogba mwenyewe, Juventus nayo imo kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumfukuzia staa huyo.

 

Manchester United sasa wamekubali yaishe na wameamua kuweka wazi kuwa klabu inayomtaka inatakiwa kutoa kiasi cha pauni milioni 150 (Sh. bilioni 436). Klabu hiyo, ambayo bado ingependa kubaki na Pogba na wameweka bei hiyo ili kupunguza kasi ya kumwania nyota huyo ingawa itakuwa ngumu kukataa fedha ikiwa itatokea klabu itakayotoa.

 

Real Madrid na Juventus, hata  hivyo, zina imani kuwa bei hiyo inaweza kupungua kutokana na ukweli kuwa Pogba mwenyewe anataka kuondoka, Pogba inaaminika hana furaha Manchester United ambapo ikumbukwe alikuwa na misukosuko mingi timu hiyo ilipokuwa chini ya kocha Jose Mourinho ingawa baadae kulikuwa na unafuu kufuatia ujio wa Ole Gunnar Solskjaer lakini matokeo yalibakia kuwa mabaya.

TCRA Watoa Neno Kuhusu Usajili wa Laini, Yatoa Onyo kwa WANANCHI

Comments are closed.