The House of Favourite Newspapers

DC Gondwe: Tuache Maneno, Tufanye Kazi – Video

0

WAKAZI wa Wilaya ya Temeke wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kuhakikisha maeneo yake yanakuwa katika hali ya usafi.

 

Wito huo ulitolewa jana, Januari 10, 2021, na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe,  wakati akizungumza na viongozi  na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Stereo alipolitembelea ili kukagua hali ya usafi katika eneo lote la soko na mitaa ya jirani yake.

 

Pamoja na kusisitiza watu kufanya kazi, alisema iko haja ya kuwa na siku ya kufanya usafi kwa pamoja wilayani humo.

 

“Nyinyi viongozi nendeni mkakae na wafanyabiashara wenzenu wa soko hili mjadiliane, mpange muda wa usafi wa pamoja. Siku tuliyoipitisha kwa ajili ya usafi ni Jumamosi, na katika maeneo mengine, tumepanga muda wa kuanzia saa 12 mpaka saa 3 asubuhi… Tuache maneno, tufanye kazi.

“Lakini kutokana na asili ya hapa, hatutaki kuwaingilia, angalieni wenyewe ni muda gani utafaa, kubalianeni. Ninachotaka,ni usafi ufanyike. Uhai hauna mbadala ndugu zangu,” alisisitiza Gondwe.

 

Kiongozi huyo ameendelea kukagua usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya wilaya yake, ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi wa mazingira kiwilaya, iliyofanyika mwezi Novemba 2020 katika eneo la Mbagala Rangi Tatu.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

 

Leave A Reply