The House of Favourite Newspapers

TUHUMA ZA KUMKWAMISHA JPM, MEMBE AMJIBU DKT. BASHIRU

BAADA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally akumtaka mwanachama wa chama hicho, Bernard Membe kufika ofisini kwake ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma za kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli, mwanadiplomasia huyo amemjibu Katibu Mkuu huyo na kusema atakwenda kumuona licha ya kudai kushangazwa na utaratibu uliyotumika kumuita.

 

Membe ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje na mgombea urais wa mwaka 2015, amesema kuwa amemueleza Dkt. Bashiru siku atakapofika ofisini hapo, pia Cyprian Musiba awepo ili kuthibitisha tuhuma hizo kwani ndiye aliyeziibua  kupitia Gazeti lake la Tanzanite.

 

Comments are closed.