The House of Favourite Newspapers

Tume ya Madini Yafanya Makubwa

0

Tume ya Madini imefikia lengo kukusanya maduhuli kwa zaidi ya asilimia 100. Katika 2018/19 ilikusanya maduhuli ya sh bilioni 346.78 sawa na asilimia 101.59 na kuvuka lengo la kukusanya Sh bilioni 310.32. Katika 2019/20, Tume hii imevuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 470.35 sawa na asilimia 112.31 ya lengo la kukusanya sh bilioni 528.24.

 

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Profesa Idrisa Kikula alieleza mafanikio hayo kwenye mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Sekta ya Madini uliofanyika jana.

 

Profesa Kikula alisema, Tume hiyo yenye wafanyakazi 68 imevuka malengo katika kukusanya maduhuli mwaka 2018/19 na 2019/20 yaliyowekwa na wizara ambapo katika 2018/19 ilikusanya maduhuli ya sh bilioni 346.78 sawa na asilimia 101.59 na kuvuka lengo la kukusanya Sh bilioni 310.32.

 

“Tume ya Madini Tanzania imeongeza idadi ya masoko na vituo vya kuuzia madini kutoka masoko 31 na vituo 38 katika mwaka 2019/20 hadi masoko 39 na vituo 50 hadi Aprili, 2021.

 

“Pia katika 2019/20, tume hii imevuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 470.35 sawa na asilimia 112.31 ya lengo la kukusanya sh bilioni 528.24.

 

Tume ya Madini imeongeza idadi ya utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji madini ambapo 2019/20 ilitoa leseni 5,935 na tangu Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu 2021, imetoa leseni za utafutaji na uchimbaji madini 8,709,” alisema.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akifungua mkutano huo alisema wizara hiyo inatambua mchango mkubwa wa tume hiyo katika kuhakikisha raslimali ya madini inawanufaisha watanzania na taifa kwa ujumla.

Leave A Reply