The House of Favourite Newspapers

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kutambulika Rasmi Kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

0

Tume ya Uchaguzi (NEC) itabadilishwa jina ifikapo Aprili 12, 2024 ambapo sasa itaanza kutambulika kama Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi imesema hatua hiyo inafuatia tangazo la Serikali namba 225 la Machi 29, 2024 la Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba 2 ya mwaka 2024, inayoanza kutumika rasmi Aprili 12, 2024

Msemaji Mkuu amesema “Hivyo, kuanzia Aprili 12, 2024 jina la Tume litabadilika na litakuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi au kwa kiingereza ‘Independent National Electoral Commission’,”

Ikumbukwe, Mabadiliko hayo yanakuja baada ya Bunge la Tanzania kupitisha Miswada ya Sheria za Uchaguzi ambazo zimesainiwa na kuridhiwa na Rais Samia Suluhu Hassan



 

Leave A Reply