The House of Favourite Newspapers

TUNDA AJIPANGA KURUDI SHULE

Anna Kimario ‘Tunda’

MREMBO aliyejipatia umaarufu kupitia video za wasanii mbalimbali pamoja na matukio kwenye mitandao ya kijamii, Anna Kimario ‘Tunda’ ameeleza kuwa, anajipanga kurudi shule ili kujiongezea elimu.

 

Akichonga na Risasi Jumamosi hivi karibuni mrembo huyo amesema kuwa, lengo lake ni kuwa mtaalam wa mambo ya kompyuta hivyo anataka akasomee kozi ya Information Technology (IT).

 

Mrembo huyo anakiri kwamba, ameshapoteza muda mwingi kwenye mambo yasiyo sahihi na sasa ameona bora arudi shule kwani umri unamruhusu kuwa na maisha tofauti na aliyonayo sasa. “Siku zote napenda kusomea kozi ya IT, ni kitu kilichopo kwenye ndoto yangu na kwa sababu sasa nimekua na kutulia, naamini nitasoma kwa utulivu kabisa,” alisema Tunda.

STORI: Imelda Mtema

 

DIAMOND ATUA SUMBAWANGA KWA NDEGE, MAPOKEZI YAKE BALAA! (VIDEO)

                  PART 1

 

                 PART 2

Comments are closed.