The House of Favourite Newspapers

DIAMOND APEWA SHULE SUMBAWANGA – VIDEO

Msanii Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz akicheza na wamama wa Sumbawanga.

Msanii Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameweka jiwe la msingi na kukabidhiwa Shule ya Senti ambayo wamemuomba iitwe jina la Diamond katika Mtaa wa Senti wilayani Sumbawanga leo, Jumamosi, Desemba 8, 2018.

Diamond amefanya tukio hilo alipokuwa ametembelea wilaya hiyo kwenye ziara yake ya muziki, ‘Wasafi Festival’ ambalo linategemewa kufanyika leo. Mradi wa shule hiyo umepungukiwa na kiasi cha Tsh. Million 68 ili kuweza kukamilika na shule ifunguliwe ifikapo Januari 2019.

 

Aidha, Diamond ameahidi kwamba kwa kiasi kilichobaki Watamalizia wote, “Mimi nathamini sana elimu na niwaahidi kitu kimoja kwamba, ujenzi huu uliyobaki, nitaumalizia wote,” aliahidi Diamond kwa wananchi mbele ya uongozi wa shule hiyo.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

TAZAMA VIDEO NZIMA

Comments are closed.