The House of Favourite Newspapers

TUNDA, LYINN VITA MPYAA KWA DIAMOND

MAHABA kama yotee! Kipande cha video kilichosambaa kwenye mitandao ya kijamii kikimuonesha video queen matata wa Bongo, Annastazia Sebastian Kimaro ‘Tunda’ akimkatia mauno staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imezua vita mpya.

NI KATI YA TUNDA NA LYNN

Vita iliyoibuliwa na video hiyo ni kati ya mhusika Tunda na video queen mwenzake, Irene Hilary ‘Lynn’ ambao wote wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond.

Tukio hilo la kurekodiwa kwa video hiyo ya Tunda akimpa utamu wa mauno Diamond lilijiri usiku wa Oktoba 2, mwaka huu kwenye pati ya bethidei ya Diamond iliyofanyika nyumbani kwa mmoja wa mameneja wake, Salam SK maeneo ya Masaki jijini Dar.

TUNDA NA DIAMOND

Kwa muda mrefu Tunda alisemekana kuwa na ukaribu wa kimapenzi na Diamond kiasi cha kudaiwa kunasa ujauzito wa jamaa huyo ambao baadaye ulichoropoka.

Kufuatia madai hayo, miezi kadhaa iliyopita, Tunda na Diamond walikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi zaidi ya kikazi. “Kwa nini kila mwanamke mzuri ninaambiwa ninatoka naye mimi tu? Au mimi nina asali? Sina uhusiano na Tunda,” alikaririwa Diamond.

VIDEO YA JUZIKATI

Baada ya ukimya wa muda huku Diamond akiendelea na sarakasi nyingine za wanawake, ndipo juzikati kukazuka hili la kukatikiwa mauno na Tunda usiku mnene kabla ya kudaiwa kuondoka wote na kwenda kubarizi kusikojulikana.

VITA MPYA NA LYNN

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na mrembo Lynn ambaye haambiliki kwa Diamond, mara baada ya kusambaa kwa video hiyo ndipo lilipotangazwa bifu jipya mjini kati ya Tunda na Lynn.“Si unajua ni juzi tu Lynn alidaiwa kuzawadiwa mpaka gari na Chibu (Diamond) wakati wa bethidei yake?

“Sasa hiyo video ya Tunda imemtibua Lynn na timu yake kwa sababu Lynn humwambii kitu kwa Diamond ‘so’ sasa hivi ni mwendo wa vijembe tu huko social media (mitandao ya kijamii). “Wenyewe wanasema kama mwanamke akitaka kumtibua Lynn, basi ajisogeze kwa Diamond kama alivyofanya Tunda maana ameshasema kuwa yupo tayari kuolewa na jamaa huyo, sasa hataki mtu amtibulie,” kilidai chanzo chetu hicho cha kuaminika.

TUNDA ABANWA, AELEZA

Baada ya kupata ishu hiyo, Ijumaa lilimtafuta Tunda na kumbana juu ya video hiyo na kwamba imesababisha vita mpya kati yake na Lynn ambapo alifunguka:

“Jamani kama ujuavyo ile ilikuwa ni sherehe na kila mtu pale alikuwa ameshakunywa (amelewa) na wengi walikuwa wanacheza, nashangaa sana wameniona mimi tu ndiye nilikuwa nacheza na Diamond, kama siyo mambo ya ajabu ni nini?” Tunda alisema kuwa anashangaa mno yeye kumpa mauno Diamond ndiyo imekuwa maneno maana watu wengi walicheza naye, lakini video zao hazikurushwa mtandaoni na kusababisha taharuki.

“Mimi kucheza na Diamond imekuwa ishu kubwa, kitu ambacho kinanishangaza sana. “Ina maana watu waliniona mimi tu? Lakini mimi naona ni kitu cha kawaida kabisa kwangu hivyo watu wasipate tabu sana,” alisema Tunda. Alipoulizwa kuhusu mwanaume wake anasemaje juu ya video hiyo, Tunda alisema kuwa, kwa sasa hana mtu anayemhofia kwani alishaachana na Casto Dickson muda mrefu.

“Mimi sijali kama wanasema, waseme tu kwani sina muda na mtu,” alisema Tunda. Alipoambiwa kuwa video hiyo imesababisha vita mpya kati yake na Lynn, Tunda alisema hajui wala hana muda wa bifu na mtu.,Ijumaa lilipomtafuta Lynn na kumuuliza juu ya sakata hilo hakutaka kulizungumzia.

Tunda na Lynn ni warembo ambao wote walishauza sura kwenye video za Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond ndipo walipopata ukaribu na jamaa huyo. Tunda aliuza sura kwenye video ya Wimbo wa Salome wa Diamond na Rayvanny huku Lynn akionekana kwenye video ya Wimbo wa Kwetu wa Rayvanny, zote za WCB.

Comments are closed.