Tunda: Moyo Wangu unapenda Kuishi Hotelini

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii pendwa ya My Style, kama ilivyo kawaida tunakuletea mastaa mbalimbali ambao huzungumzia maisha yao na vitu wanavyovipenda.

 

Leo tunaye Video Vixien, Anna Kimario ‘Tunda’, ambaye amefunguka vitu mbalimbali katika mahojiano aliyoyafanya na safu hii kama ifuatavyo…

Risasi Jumamosi: Kabla hatujaenda mbali naweza kujua ni kwa nini uliitwa Tunda? Tunda: Nilipokuwa mdogo, watu walikuwa wakinipenda na wengine walikuwa wakipenda kunisifia kuwa ni mzuri, wakawa wananiita Tunda na jina hilo likazoeleka mpaka leo hii.

 

Risasi Jumamosi: Umekuwa ukionekana hotelini mara kwa mara watu wanajiuliza hapa jijini Dar huna nyumbani kwenu au hujapanga nyumba kwa sababu hujawahi kuonekana nyumbani?

 

Tunda: Unajua mimi napenda sana kuipa nafsi yangu furaha na siyo ya mtu mwingine, hapa nina kwetu lakini napenda kuishi hotelini kwani moyo wangu ndio unavyotaka.

 

Risasi Jumamosi: Hotelini mara nyingi mnapikiwa vyakula na kufanyiwa kila kitu, wewe ni mwanamke huoni kama utalisahau jiko?

Tunda: Kama unajua kupika, unajua tu siwezi kusahau hata siku moja na hata hivyo siyo maisha yangu, mara nyingi nikitupia picha watu hutafsiri kuwa picha hiyo ni ya muda huohuo lakini siyo kweli.

 

Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu mpenzi wako Whozu, mko kwenye mapenzi ya kweli au mnaigiza?

Tunda: Asikwambie mtu pale nimenasa, nampenda wala hakuna kuigiza kabisa. Risasi Jumamosi: Ukitoka unapendelea kuvaa mavazi gani?

 

Tunda: Kwa kweli mimi kwa yeyote anayenifahamu anajua sipendi kujibebesha mavitu kwenye mwili wangu, napendelea kupigilia simpo ila huwa navaa vitu venye ubora.

 

Risasi Jumamosi: Kwa upande wa kichwa je, hupendelea mtindo gani maana mara nyingi umekuwa ukionekana na nywele fupi?

Tunda: Tangu nakua sikuwa napendelea nywele, na hata kichwani kwangu naweza kusuka leo kesho nanyoa, kifupi napenda nywele fupi.

 

Risasi Jumamosi: Unapendelea kula chakula gani, je huwa unapika?

Tunda: Nikiwa nyumbani napenda chakula cha kawaida kama wali maharage pia huwa napenda sana kupika na napenda kupika pilau, nikipika kila mtu anakula na kuomba nirudie kwani utamu wake si mchezo.

 

Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu wazazi wanakuchukuliaje wanapoona mambo yako kwenye mitandao ya kijamii?

Tunda: Unajua familia yangu inanijua mimi vizuri kuliko mtu yoyote yule, hivyo hawaoni kama kuna tatizo, wanaelewa.

Risasi Jumamosi: Nini unachokipendelea zaidi?

 

Tunda: Napenda sana kutulia sehemu nzuri na yenye mandhari ya kupendeza, huku nikitazama bahari.

Risasi Jumamosi: Je, una mpango wa kuzaa na mpenzi wako Whozu? Tunda: Ndiyo tena watoto pacha.

Risasi Jumamosi: Haya asante sana Tunda. Tunda: Asante, karibu sana.

MAKALA: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment