The House of Favourite Newspapers

Tundu Lissu Aandika Historia TLS… Ashinda Urais kwa Asilimia 88

Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo wamefanya uchaguzi wa kumchagua rais pamoja na wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama chao.

Tundu Lissu inaelezwa kwamba ameshinda urais wa Chama cha Wanasheria (TLS) uliokuwa ukifanyika Arusha, leo kwa zaidi ya 88% ya kura zote.
Uchaguzi huo umefanyika mjini Arusha ambako wanachama  wa TLS wamekutana kutekeleza ratiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji kazi wa chama hicho.
Matokeo ni kama ifuatavyo:
 
Urais: Kura zilizopigwa 1682
  1.     Tundu Lissu 1411  sawa na asilimia 88
  2.     Francis Stolla 64
  3.     Victoria Mandari 176
  4.     Godwin Mwapongo 64
==>Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.
 
Council Members
  1.     Jeremiah Motebesya
  2.     Gida Lambaji
  3.     Hussein Mtembwa
  4.     Aisha Sinda
  5.     Steven Axweso
  6.     David Shilatu
  7.     Daniel Bushele

Comments are closed.