Tundu Lissu Asomewa Mashtaka 5 Kisutu, Aachiwa kwa Dhamana, Akwea Pipa Kuelekea Arusha

   

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari mara baada ya kupata dhamana Mahakama ya Kisutu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Mbunge Tundu Lissu aliyefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matano.

Mama mzazi wa Wema Sepetu, Mariam Sepetu naye akitoka kusikiliza kesi hiyo.

Lissu amesomewa Mashitaka matano(5)  ambayo ni yale yale aliyofutiwa hapo awali kuhusu maneno ya Uchochezi kwenye Uchaguzi wa Dimani, Zanzibar.

Lissu alipofikishwa Mahakamani leo asubuhi kusikiliza kesi inayomkabili.

Serikali imesema upelelezi umekamilika na   ikaomba kesi ianze kusikilizwa leo.Lissu aliiomba mahakama isisikilize  kesi hii  leo ili akashiriki Uchaguzi wa TLS utakaofanyika kesho mkoani Arusha.

Mbunge wa Arusha mjini, Godbles Lema akizungumza jambo mara baada ya kutoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

Mahakama imekubali maombi ya Tundu Lissu na kumwachia huru kwa dhamana ya milioni 10 ambapo tayari amekwishapanda ndege kuelekea jijini Arusha Kushiriki Uchaguzi huo

 

Denis Mtima/GPL


Loading...

Toa comment