The House of Favourite Newspapers

Tuzo Za Mwaka Huu Si Mchezo, Joti Na Mkojani Walivyotifuana Filamu Za Vichekesho

0
Joti (kulia) alivyoenda kupokea tuzo yake kwa mbwembwe na madaha.

Wasanii mahiri wa filamu za vikesho hapa nchini, Mkojani na Joti usiku wa kuamkia leo walitifuana vikali kwenye tamasha la Tuzo za Filamu 2023 lililofanyika The Super Dome Masaki, Dar.

Mkojani akizungumzia tuzo zake.

Mara kadhaa wasanii hao walitajwa kuwania kipengele kimoja upande wa filamu za vichekesho ambapo awali walipotajwa wasanii hao macho ya wengi yalikuwa yakisikiliza tuzo hiyo ilikuwa ikienda kwa staa yupi kati yao.

Hata hivyo mwisho wa siku Mkojani aliibuka na tuzo mbili huku Joti akiibuka na tuzo moja ambapo wasanii hao kipenzi cha mashabiki yalisikika mayowe ya aina yale kila walipotajwa kwenda kuchukua tuzo.  Tamasha hilo limeandaliwa na Wizara ya Sanaa na Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS GLOBAL

Leave A Reply