The House of Favourite Newspapers

Usiku wa Tamasha la Tuzo Za Filamu Wafana Dar, Underground Ben Royal Awafunika Mastaa Na Tuzo 6

0
Ben Royal akiwa na tuzo zake sita alizojizolea kwenye tamasha la tuzo za filamu 2023.

Tamasha la Usiku wa Tuzo za Filamu lililoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini na kufanyika Ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar, usiku wa kuamkia leo limesifiwa na wadau kwa jinsi lilivyofana na kuvunja rekodi ya miaka mitatu iliyopita lilipoanzishwa huku muongozaji wa filamu chipukizi kutoka Mbeya Ben Royal akiwafunika Mastaa kwa kuzoa tuzo sita.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akimpa heshima yake Ben Royal.

Katika tamasha hilo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliyeambatana Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa na viongozi wengine wa kisiasa.

Ben Royal akifurahia tuzo hizo na wasanii wenzake wa Royal Family.

Kipute cha kuwania tuzo hizo kilikuwa na vita kali ya lakini msanii mwisho wa yote muongozaji chipukizi wa filamu kutoka kundi la Royal Family la mkoani Mbeya, Benard Edson maarufu kama Ben Royal ndiye aliyewafunika wote wakiwemo mastaa kwa kuzoa tuzo sita ambazo ni, Best Director, Best Best Feature Film, Best Editing, Best Effect, Best Sound na Best Key Play.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL

Leave A Reply