The House of Favourite Newspapers

Twalib Mchezaji Wa Zamani Wa Simba Agawa Misaada Kwa Yatima Kuelekea Mfungo Mtukufu Wa Ramadhani – Video

0


TALIB Hilal mshauri wa Ufundi wa Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ambaye alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Simba ametoa sadaka kwa makundi maalumu kuelekea mfungo mtukufu wa Ramadhani.

Hii ni mara ya tano kwa kocha huyo wa timu ya taifa ya ufukweni ya Oman kufanya hivyo akiweka wazi kuwa imani ya dini inasema kuwa kama unacho ni muhimu kutoa na unapopata gawana na mwenzako.

Talib amekuwa akishirikiana na Global Publishers katika suala la kuwakumbuka watoto yatima. Na aliongozana na msaidizi wake, Yusuph Abeid, kipa wa zamani wa Pamba ya Mwanza.

Talib ameweka wazi kuwa kinachopatikana japo kidogo tunagawana na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu atufungulie kila lililo kheri.

Leave A Reply