The House of Favourite Newspapers

Twanga Ilivyokinukisha Onesho La Krisimasi Uspime

0

Kiongozi wa wanenguaji wa Twanga Super Nyamwela (katikati) akicheza staili ya Maria Roza na Stellah Kiuno (kushoto) na Maria Soloma.

Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa kuamkia leo ilifanya onesho la Krisimasi ndani ya Ukumbi wa KB uliopo Tabata Bima Jijini Dar ambapo mambo yalikuwa si mchezo. Wakati Wana hao wa kutwanga na kupepeta wakifanya yao mashabiki nao walijimwaya kwa raha zao wakifurahia Sikukuu hiyo. Baada ya kumaliza shoo hiyo bendi hiyo iliunganisha Kahama mkoani Shinyanga ambapo itakuwa na shoo za muendelezo kanda hiyo ya ziwa. Angalia picha.

Shabiki akijiachia kwa selfie na Luiza Mbutu (kulia) na Kalala Junior.
Mnenguaji Stellah Kiuno akifanya yake.
Mwanamuziki wa Twanga, Khalid Chokoraa akifanya yake na mashabiki.
Mcharaza solo gitaa, Miraj Shakashia  akiwajibika.

HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply