The House of Favourite Newspapers

Uhondo wa Krisimasi Ndani ya Dar Live Waacha Gumzo

0

USIKU wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live kulikuwa na bonge la shangwe katika kusherehekea Sikukuu ya Krisimasi. Burudani hiyo ilinogeshwa na wasanii wa Singeli, Bongo Fleva na Regge. Kama ilivyokuwa kawaida ya kiwanja hicho mambo yalianza mapema kabisa kwa michezo ya watoto kama vile kubembea, kuserereka, kupanda ndege, mashindano ya kuendesha baiskeli na michezo mingine mingi. Wakati watoto wakifurahia michezo hiyo watu wazima wao kama kawaida walikuwa wakiendelea na kilaji mpaka jua lilipozama watoto walirudishwa majumbani ndipo burudani za kiutu uzima zilianza kuchukua nafasi.

Mwanamuziki wa Regge, Rankim Boy a.k.a No faya akiwachizisha mashabiki na nyimbo zake za regge.
Mashabiki wakijiachia.
Shangwe ilikuwa kama zote.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply