The House of Favourite Newspapers

Twitter Kuanza Kuwatoza Ada Wafanyabiashara na Serikali, Musk Atoa Tamko Jipya

0

Wafanyabiashara na Serikali wanaotumia mtandao wa Twitter huenda wakahitajika kulipa ada kidogo ili kusalia kwenye mtandao huo wa kijamii, mkuu wa Tesla Elon Musk amesema.

 

Hii ni baada ya bodi ya Twitter kukubali ofa ya kuchukua dola bilioni 44 (£34.5bn) kutoka kwa Bw Musk.

Hata hivyo, Musk alisema mtandao huo daima uakuwa wa bure kwa “watumiaji wa kawaida”.

Hapo awali alisema anataka “kufanya Twitter kuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa kwa kuboresha muonekano wake na kujumuisha vipengele vipya”.

 

Hapo awali, Musk alikuwa ametuma kiunga cha habari ya CNN iliyotaka baadhi ya makampuni makubwa zaidi ya Marekani kususia Twitter ikiwa Musk atarejesha nyuma sera za udhibiti wa maudhui zinazozuia matamshi ya chuki.

 

Anahoji kuwa sera za udhibiti za Twitter zinatishia uhuru wa kujieleza.

Tangu kukubali kununua Twitter,  Musk amesema alitaka kufanya maboresho ili kusaidia kuongeza mvuto wa kile anachoeleza kuwa jukwaa maalumu.

Leave A Reply