The House of Favourite Newspapers

Mwanamama Mkongwe wa Muziki Stara Thomas Afunguka “Nipo Kimya Ila Ninaishi”

0
Staa wa Bongo Fleva, Stara Thomas.

WENGI nimewaona ila moyo… Watakapo tuuu kutulia… Kwa dhati ninanena  Ukweli ninasema…aahh kutoka moyoni…  Nipo kwa ajili yako wewee…  Hata kama uende mbali ohhh…

Sito linadi pendo lako…

Hivyo ndivyo nilivyo bwana weehh…

Hata kama waseme sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Hata kama wanune sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Hata kama wasuse sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Fahari ninapata uwapo karibu yangu ohh…

Kila wakati oohh…

Siku hadi siku wazidi kutulia aahh…

Moyoni mwangu…

Shaka sikutilii weweee…

Kwani jibu nimeshapata yoohh…

Nafsi imekubali nayooo…

Kipingamizi hakuna tena yoohh…

Hata kama waseme sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…”

Haya ni mashairi ya Ngoma ya Nipo Kwa Ajili Yako. Ni moja kati ya ngoma kali kutoka kwa mwanamama mkongwe muziki nchini Tanzania, mama wa makolabo, Stara Thomas.

Ni mama wa makolabo kutokana na baadhi ya ngoma zake kushirikiana na wasanii wengi na nakufanya vizuri kama Riziki ya K Basil na Bizman, Kigugumizi ya Mr Paul, Ungeniambia ya MwanaFA, Mchakamchaka ya Mr 2 a.k.a Sugu, Nipigie ya AT na nyinginezo.

Stara anasema anafurahia kufanya ngoma na msanii mwingine kuliko kufanya mwenyewe ndiyo sababu nyimbo zake zote alizoshirikishwa au kumshirikisha msanii yeyote, watu wanazifurahia na yeye mwenyewe anazipenda.

Stara anayasema hayo kutokana kurudi tena rasmi kwenye muziki Bongo Fleva baada ya kufanya muziki wa Injili na kufanikiwa kutoa album moja ya Nani Mshamba.

Anasema hivi sasa anafanya kazi zaidi kwa kushirikiana na wasanii wengine kwa sababu anapenda umoja.

Anasema mikakati yake aliyonayo hivi sasa ni kuachia nyimbo zake back to back ili kuweza kurudisha mashabiki wake kama zamani ingawa anaamini kwamba hawajapotea kutokana na ngoma zake zinavyoishi.

 

Kuhusu album anasema kuwa alishauriwa kufanya hivyo, lakini halifikirii hilo kwa sasa kwani hakuna mabadiliko yoyote sokoni.
Stara ana album mbili za Bongo Fleva za Nyuma Sitarudi na Hadithi.

Stara alianza kufanya vizuri miaka 10 iliyopita na nyimbo zake kama Mi na Wewe, Nakupenda, Wasiwasi na nyingine kibao.

 

IJUMAA limefanya mahojiano maalum (exclusive) na Stara ambaye anafunguka mambo mengi kuanzia sababu za ukimya wake na mengine mengi;

 

IJUMAA: Mambo vipi Stara?

STARA: Salama kabisa.

IJUMAA: Bado unawake ile mbaya, hebu tupe siri ni nini?

 

STARA: Unajua pale ambapo unakubali kuishi maisha yako ya uhalisia, huwezi kuzeeka haraka japo kuna mawazo ya hapa na pale, lakini ukitaka kuwa mzuri muda wote, usipende kujichanganya kwenye vitu ambavyo vinachosha mwili.

 

IJUMAA: Hivi unaweza ukawa na miaka mingapi?

STARA: Hilo ni swali nakuachia kuweza kubuni mimi nina miaka mingapi sasa…(kicheko kidogo).

IJUMAA: Naona kwenye miaka arobaini na kitu…

STARA: Ndiyo hivyo hiyo arobaini na kitu.

IJUMAA: Maisha kwa sasa yanasamaje maana ni muda umepotea kwenye gemu?

 

STARA: Maisha yanaendelea vizuri, japokuwa kuna milima na mabonde, lakini maisha lazima yaendelee.

IJUMAA: Upo kimya sana kwa muda mrefu sababu ni nini hasa?

 

STARA: Nipo kimya kweli, lakini ngoma zangu zipo na zinapigwa sana, ndiyo maana unaweza ukaona Stara nipo kimya, lakini hizo nyimbo mimi ndiyo zinanifanya nakumbukwa na zinaishi, ninafanya nazo kazi mpaka sasa na sasa nipo ninarekodi nyimbo.

 

IJUMAA: Tunaona pia kuna ngoma mpya umeachia na Banana Zorro ya Sogea Karibu; hii ni baada ya miaka kama mingapi hivi?

 

STARA: Ni miaka 10 sasa.

IJUMAA: Tunafahamu kwamba msanii akitaka kurudi kileleni, lazima ajibosti na msanii ambaye yupo ‘on-trending’, kwa nini usingeimba na Harmonize au Diamond, badala yake ukamchukua Banana?

 

STARA: Nimemchukua Banana kutokana na umri, lakini pia kufanya hivyo ni vizuri, ila mimi kama Stara ninatosha, nadhani zinaweza zikaja kolabo yangu na Diamond pamoja na Harmonize mipango hiyo ipo.

 

IJUMAA: Tukirudi kidogo kwenye familia, vipi watoto wamekua?

STARA: Ndiyo wamekua.

IJUMAA: Una watoto wangapi?

 

STARA: Nina watatu kwa sasa, bahati mbaya kaka yao alitangulia mbele za haki.

IJUMAA: Polesana, je, uliona posti ya Ruby ambayo alikuwa akisema kwamba anatamani kufa, wewe unazungumziaje juu ya kauli ile?

 

STARA: Kiukweli iliniumiza sana, ila ninachotaka kumwambia ni kwamba akazane na maombi, hakuna linaloshindikana mbele za Mungu.

IJUMAA: Mahusiano yamekuwa yakiwasumbua wasanii wa kike kwa sasa hasa Ruby wewe unaonaje?

 

STARA: Kwanza mimi sina muda wa kuremba maisha yangu, likija jambo kama siliwezi naachana nalo, mimi niliingia kwenye mahusiano nikiwa tayari nina majibu, inawezekana wengine wanaingia wakiwa bado hawajajipanga

 

IJUMAA: Kuna kipindi tulisikia kwamba umeacha muziki na umeamua kuimba kwaya, bado unaimba kwaya?

STARA: Ndiyo bado nafanya kwa sababu kwangu kwaya ni ibada.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Umerudi sasa, je, mashabiki wako wategemee nini?

 

STARA: Katika ujio huu wa sasa, nitatoa nafasi kwa watu wenye vipaji vya kuandika, kuna watu wana uwezo wa kuandika nyimbo, lakini hawajapata nafasi, mimi nataka niwasaidie, niko tayari kuandikiwa na mtu yeyote ili nao vipaji vyao vitambuliwe.

 

IJUMAA: Kuekea Mei 14, mwaka huu ambayo ni siku yenu wakongwe unawaambia nini mashabiki wako?

STARA: Waje kwa wingi waone mambo yanavyofanyika.

Leave A Reply