Twitter Yawatimua Kazi Mameneja Wawili Kupisha Utawala wa Elon Musk

Mkurugenzi Mkuu wa Twitter Parag Agrawal

TWITTER imewatimua kazi Mameneja wawili wa ngazi ya juu na kusitisha ajira ikiwa ni mpango wake wa mabadiliko chini ya utawala mpya wa bilionea namba moja duniani Elon Musk.

 

Mtandao huo wa kijamii umethibitisha kuondoka kwa Meneja Mkuu Kayvon Beykpour na Mkuu wa bidhaa na kodi Bruce Falck na kusisitiza kuwa ajira itauwa ni kwenye maeneo muhimu tu huku ikisubiri kipindi cha mabadiliko chini ya utawala wa Elon Musk.

 

Wote wawili walithibitisha kuwa wameondolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Twitter Parag Agrawal.

Kayvon Beykpour Meneja Mkuu aliyetimuliwa kazi kwenye Kampuni ya Twitter

“Parag aliniambia niondoke baada ya kunijulisha kuwa anataka kuipeleka timu katika uelekeo mwingine.” Alituma ujumbe huo Beykpour kupitia mtandao wa Twiiter na kuongeza kuwa wakati anatimuliwa kazi alikuwa katika likizo ya uzazi.

Elon Musk Bilionea namba moja duniani na mmiliki wa Twitter

Nafasi ya Agrawal mwenyewe ipo katika hatari kubwa ya kuchukuliwa na Elon Musk ambaye ni mmiliki mpya wa Twitter, hisa za kampuni hiuo zilishuka kwa 3% siku ya alhamis na kusababisha hasara ya dola milioni 10.

Elon Musk amerudia mara kwa mara kuthibitisha adhima yake ya kuitaka Twitter kuwa jukwaa la uhuru wa kujieleza na kupunguza utegemezi wa matangazo ya biashara kama njia ya kuendesha na kuingiza mapato ya kampuni hiyo.

 

 706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment