The House of Favourite Newspapers

Tyson Fury Alivyomkalisha Wilder Raundi ya Saba – Video

0


Bondia Tyson Fury ametwaa mkanda wa uzito wa juu duniani wa WBC baada ya kumtwanga kwa TKO Mmarekani Deontay Wilder katika pambano la raundi 12 lililochezwa leo katika ukumbi wa MGM Grand Arena, Las Vegas, Nevada, Marekani.

 

The Gypsy King ambaye aliingia kwenye pambano hilo akiwa amevaa kifalme kwa ushindi huo amempora Wilder mkanda wa WBC na amefanikiwa kutwaa mkanda wa Ring Magazine ambao haukuwa na mwenyewe.

 

Fury bingwa wa zamani wa uzito wa juu wa WBA, WBO, IBF na IBO, alitawala pambano hilo na kumshambulia Wilder tangu kengere ya kwanza huku akimpa wakati mgumu Mmarekani huyo kutumia mkono wake wa kulia ambao umekuwa ukimpa ushindi.

Leave A Reply