The House of Favourite Newspapers

Uamuzi wa Kesi ya Akina Halima Mdee, Wenzake Washindwa Kutolewa..

0

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha kutoa uamuzi wa maombi ya Halima Mdee na wenzake 18 ya kutaka kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hadi Ijumaa ya Julai 8, 2022 kutokana na Jaji kutokuwa amemaliza kuandaa uamuzi huo.

 

Jaji anayesikiliza shauri hilo  Jaji Mustapha Ismail alikuwa atoe aumuzi huo lakini Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Elimo Massawe amesema, haujakamilika na utatolewa Ijumaa hii.

 

Mdee na wenzake wanaomba ridhaa ya kupinga uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA wa Mei 11, 2022 kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama, yaani ipitie uamuzi wa Chadema kisha itoe amri mbili.

Leave A Reply