The House of Favourite Newspapers

Makamba Atia Neno Uba Kuja na Huduma za Facebook App

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muugano na Mazingira  Janauary Makamba,(wapili kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa  United Bank For Africa(UBA) Kusini na Mahariki mwa Afrika ,Emeke Iweriebor   (kushoto) Mwenyekiti wa bodi ya UBA, Balozi Tavuko Manongi  (watatu) na Mkurugenzi Mkuu wa UBA nchini , Usman Isiaka wakimsikiliza kwa makini  Mkuu wa kitengo Huduma za kibenki  kwa njia ya Kidijitali wa UBA,Asupya Nalingiwa
Waziri makamba akiwaongeza viongozi wa benki hiyo.
Mmoja wa viongozi wa benki hiyo akizungumza jambo katika hafla hiyo.

 

 

United Bank for Africa (UBA) leo imezindua huduma mpya ya chatbot inayojulikana kama LEO ikiwa ni ya kwanza na ya aina yake kwa hapa Tanzania.

 

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Kusini na Mashariki mwa Afrika, Bw. Emeke E. Iweriebor alisema, “kupitia huduma hiyo mpya, wateja wa benki ya UBA wataweza kutumia Facebook kufanya miamala ya kibenki kwa urahisi na usalama”.

 

 

Alisema uamuzi huo umechochewa na takwimu zinazoonyesha kuwa tangu ilipozinduliwa huduma hiyo na UBA Group January 2018, wateja milioni 35 wamefikiwa huku miamala 500,000 ikiwa imefanyika kati ya wateja 300,000.

 

 

“Mitandao ya Facebook na WhatsApp inatumika sana kama njia ya mawasiliano siyo tu na Watanzania, bali na mamilioni ya watu duniani kote.

UBA imeamua kutengeneza utaratibu ambapo watumiaji wa mitandao hii ya kijamii wanaweza kupata huduma za kibenki zenye ubora wa hali ya juu,” alisema Emeke.

 

Aliongeza, “hii inamaanisha kuwa wateja wetu wanaweza kuchati na ndugu jamaa na  marafiki na pia kuchati na benki yake na kupata huduma za kibenki ikiwemo kujua salio, kulipia bili, kununua muda wa maongezi, kuangalia statement, kutuma pesa na hata kuangalia msimamo wa ligi za mpira na huduma nyingine nyingi.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano January Makamba aliyekuwa mgeni rasmi alisema uamuzi wa kuzindua huduma hiyo hapa nchini, utawarahisishia wateja wa benki hiyo kupata huduma za kibenki.

 

 

“Mitandao ya kijamii inawatumiaji wengi sana hapa Tanzania. Kuwawezesha watumiaji wake kupata huduma za kibenki kupitia mitandao hiyo ambayo ni sehemu ya maisha yao ya kila siku maana yake ni kuwarahisishia na kuwasogezea karibu zaidi huduma za kibenki,” alisema.

 

 

Aliipongeza UBA Tanzania kuja na huduma hiyo ya kibunifu, na kutaka taasisi nyingine zinazotoa huduma za kifedha kubuni huduma zitakazoweza kurahisisha huduma za kifedha jambo ambalo litawavutia wasiotumia huduma za kibenki kufanya hivyo.

 

 

“Idadi ya Watanzania wenye akauniti za benki bado ni ndogo sana. Nimefurahi kusikia kuwa mtumiaji wa mitandao wa Facebook na Whatsup anaweza kufungua akaunti ya UBA kwa kutumia simu au kompyuta yake popote alipo. Hii itasaidia kuongeza watumiaji wa huduma za kibenki,” aliongeza.

 

 

Huduma ya LEO tayari imezinduliwa na inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika nchi 15 za Afrika ambazo ni Nigeria, Kenya, Uganda, DRC Congo, Zambia, Mozambique, Congo Brazzaville, Gabon, Cameroon, Senegal, Burkina Faso, Guinea, Ivory Coast and Benin.

 

 

“Baada ya uzinduzi huu, wateja wote na wasio wateja wa UBA wataweza kutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kufanya miamala ya kibenki kama vile kufungua akaunti mpya na UBA kupitia facebook kupitia simu, laptop, tablet au kwa njia nyingine,” alisema Usman Imam Isiaka, Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania.

 

 

Inachofanya UBA, ni kutumia ubunifu wa teknolojia kubadilisha jinsi mambo yanavyofanyika ili kwenda kidijitali zaidi kama sehemu ya maboresho mapya ya kupata huduma za kibenki. Njia hii mpya itawapa wateja urahisi na uharaka wa kupata huduma za kibenki popote walipo, bila kwenda benki,” alisema Asupya Nalingigwa, Mkuu wa Kitengo cha huduma za kibenki kwa njia ya Kidijitali.

 

 

Comments are closed.