HABARI zisizothibitishwa zimeeleza kuwa watu kadhaa wamefariki baada ya kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na Kisiwa cha Ukara katika Ziwa Victoria (wilayani Ukerewe mkoani Mwanza) kuzama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana, amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara na kwamba kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa 8:00 mchana kilipinduka.
Aidha, amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho na Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda, amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko ambapo watatoa taarifa baadaye.
Comments are closed.