The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi Serikali za Mitaa: Wilaya ya Kinondoni yatoa maelekezo

Msimamizi wa uchaguzi wa wenye viti wa serikali za mitaa kinondoni, Kiduma Siga Mageni akizungumza na waandishi wa Habari

 

Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni ametoa maelekezo kwa wananchi na wagombea kutakiwa kuyazingatia.

Akizungumza na Global Publishers, msimamizi Kiduma Siga Mageni alisema kuwa, maelekezo hayo tayari yameshabandikwa kwenye ofisi za maofisa watendaji wa Kata zote za Wilaya ya Kinondoni.

“Ni wajibu wa kila mwananchi na mgombea kwenda kwenye ofisi za afisa watendaji kuangalia maelekezo kuhusu uchaguzi kama mtu una vigezo vya kugombea. Maelekezo hayo tayari yameshabandikwa katika ofisi zote za maofisa watendaji wa Manispaa ya Kinondoni,” alisema. Uchaguzi huo wa wenyeviti wa mitaa unatarajiwa kufanyika 24/11/2019.

Imeandaliwa na Neema Adrian/ GPL

 

 

 

Comments are closed.