The House of Favourite Newspapers

Tecno yazindua duka jingine Kariakoo China Plaza

Kampuni ya Tecno inayotambulika kwa uzalishaji wa simu za viwango vya hali ya juu imezidi kutanua wigo wa soko la simu nchini Tanzania baada ya kuzindua duka jipya la simu za Tecno maarufu kama ‘TECNO Smart Hub’ Kariakoo lengo ikiwa kufikisha huduma stahiki kwa wateja wake.

Akizungumza na Global Publishers, Ofisa Uhusiano wa kampuni ya simu ya Tecno, Eric Mkomoye alisema kuwa simu hiyo ni Smart Hub ya tatu kufunguliwa nchini Tanzania na kampuni hiyo ambapo Smart Hub imekuwa ikijihusisha na uuzaji wa bidhaa za Tecno tu kama vile simu za mkononi, chaji, Battery, powerbank, cover za simu lakini pia inatoa elimu kuhusiana na utumiaji na utunzaji wa simu.

“Tecno Smart Hub itahudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja lakini vilevile kwa bidhaa zetu zina warranty ya mwaka mmoja na mwezi mmoja,” alisema Eric.

Uzinduzi huo umeambatana na tafrija fupi kutoka kwa mchekeshaji Mpoki Mjuni na michezo mingine ikiwemo Lickdraw kwa wateja walionunua simu ndani ya siku hiyo na kujishindia Fridge, TV na zawadi nyingine kibao.

Imeandaliwa na Neema Adrian/ GPL

 

Comments are closed.