The House of Favourite Newspapers

Uchawi Watikisa Nyumbani kwa Mobeto

0
Hamisa Mobeto.

WAKATI sakata lake la kuzaa na mtoto wa pili na mwanaume mwingine likiwa bado linarindima, umati wa watu ulikusanyika nyumbani anakoishi, Mbezi Jogoo jijini Dar es Salaam wiki iliyopita baada ya kudaiwa kukutwa kwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya kishirikina, Risasi linathibitisha.

Awali chanzo kimoja cha uhakika kilipiga simu chumba cha habari na kuelezwa kuwa kuna vitu vinavyotia shaka katika nyumba hiyo hivyo kutaka kwenda kuona vilikuwa ni nini.

“Jamani kuna vitu hapa havieleweki kwa kweli, ni kama uchawi si uchawi, labda mngefika mara moja muone, maana sidhani hata wenyewe kama wanajua kuhusu hili jambo,” kilisema chanzo hicho ambacho kilikataa kutaja jina lake.

Mara baada ya kufika katika nyumba hiyo, Risasi Mchanganyiko liliweza kuona vitu vilivyo-fungwa katika kabrasha, vikiwemo nazi, ndizi na dalili zote za mambo ya kishirikina.

Baada ya kuona vitu hivyo, waandishi wetu waligonga geti la nyumba hiyo na wenyeji walipotoka, waliulizwa kama wanajua kilichomo ndani ya kabrasha. Akionyesha kushtushwa, msichana aliyekutwa alipiga simu kwa Mobeto na mama yake kuwafahamisha, ambao nao walieleza kuwa wangefika hapo muda mchache unaofuata.

Mobeto alikuwa wa kwanza kuwasili eneo la tukio na baada ya kuelezwa kilichokutwa nje ya nyumba yake, alikuja juu akimtuhumu mwandishi kuwa ndiye anahusika na vitu hivyo, jambo lilisobababisha watu kujaa.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa ambaye jina lake halikupatikana mara moja aliitwa na baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, alimchukua mwandishi kwa maelezo ya kwenda naye katika vyombo vya usalama, lakini alipotoweka eneo hilo, alimwachia, akimweleza kuwa hakuwa na kosa kwa vile aliitwa na watu hivyo alikuwa akitekeleza wajibu wake.

STORI: ALLY KATALAMBULA NA BONIFACE NGUMIJE | RISASI | DAR ES SALAAM

====

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

 

====

SANCHOKA: Mwanaume Anayenitaka Lazima Awe na Vigezo Hivi!!

Leave A Reply