The House of Favourite Newspapers
gunners X

Uchebe Afunguka Kurudiana na Shilole

0

l

MUME wa msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Ashraf Uchebe amefanya mahojiano maalum (exclusive) na IJUMAA WIKIENDA, ambapo amefunguka mambo mengi likiwemo suala la uwezekano wa yeye kurudiana na bibie huyo, staa wa Bongo Fleva. Mambo yalikuwa hivi kwenye mahojiano hayo;

 

WIKIENDA: Uchebe vipi kazi zako lakini, zinaenda poa?

UCHEBE: Kabisa, Mungu ni mkubwa sana anazidi kunisimamia.

WIKIENDA: Kutokana na mambo yaliyojitokeza baina yako na mkeo Shilole mpaka kusambaa kwenye mitandao, haijaleta shida kwenye biashara yako ya gereji?

 

UCHEBE: Hapana, unajua Mungu wetu ni mwema sana na kingine wateja wa kazi yangu hawaingiliani na mambo yangu mengine kwa sababu mtu anajua akileta kitu kwangu, kinakuwa sawa lakini hawezi kuacha kwa sababu ya mambo yangu binafsi.

WIKIENDA: Ugomvi wako na mkeo umekuathiri vipi katika maisha yako ya kila siku?

 

UCHEBE: Lazima kuwe kuna mtikisiko wa hapa na pale, lakini kwa Mungu hakuna kubwa, maisha yanaendelea na tunazidi kumuomba Yeye kila siku.

WIKIENDA: Lakini chanzo cha ugomvi wenu ni nini hasa, maana watu wengi wamesikia upande mmoja tu wa Shilole?

 

UCHEBE: Unajua siku zote sio vyema kabisa kuelezea sana mambo ya mtu ambaye umeishi naye, tena mke na mume. Mara nyingi wanaume tunakubali lawama kwa sababu tunaweza kuzibeba, lakini ni vyema sana kumstiri mwanamke.

WIKIENDA: Mbona sababu kubwa ambayo hata Shilole ameielezea, kuwa umezaa nje na kingine ni yeye kutopata mtoto?

 

UCHEBE: Siku zote mimi sina tabia ya kukataa damu yangu hata kidogo na nilishasema wazi kama mtu ana mtoto wangu, amlete kwa sababu mimi nina mtoto mmoja tu na anajulikana, hivyo yeye kusema hivyo ili nionekane wa ajabu, mimi sina tatizo kama Mungu ananiona ninafaa, inatosha.

 

WIKIENDA: Lakini Uchebe, watu wengi wengependa kufahamu kile kipigo ulichompiga Shilole, ni hivi karibuni au ni siku nyingi?

UCHEBE: Siku zote mtu mwelevu anaelewa kitu kwa haraka sana na mwingine anaweza akaelewa lakini akanyamazia ukweli, lakini ngoja mimi ninyamaze tu.

 

WIKIENDA: Lakini kweli zile picha zilisosambaa mtandaoni, ni wewe ulimpiga?

UCHEBE: Inawezekana kwa sababu kwenye maisha kuna mitihani mingi sana, na kingine ni kwamba mimi sio malaika wa kufanya mema pekee, lakini pia hakuna mtu anayeweza kufanya kitu bila sababu kabisa.

 

WIKIENDA: Kuna madai pia siku ile ya Sabasaba ulimfumania na ndiyo hasa chanzo cha ugomvi mkubwa sana, japokuwa mlikuwa na matatizo mengine huko nyuma.

UCHEBE: Kweli huu ni mtihani, lakini hilo mimi siwezi kuliongelea kwa sababu maisha ya ndoa ni ya watu wawili tu na shahidi ni Mungu pekee.

Kwa hiyo, ni bora kuendelea kunyamaza ili nionekane bora kwa Mungu kuliko kwa binadamu.

WIKIENDA: Mpaka sasa ushampa takala Shilole?

 

UCHEBE: Kwa kweli hilo siwezi kuliongelea sana na siku zote naomba heri badala ya shari.

WIKIENDA: Inadaiwa pia sababu kubwa ulikuwa huwapendi watoto wake na ulishatamka sio watoto wako.

UCHEBE: Ndiyo maana nasema jalala linapokea kila baya, hivyo mimi naomba nipokee hilo kwa sababu kwa sasa ni wakati wake, ila wakati wangu Mungu anauandaa.

 

WIKIENDA: Sasa akikufuata kwa sasa na kutaka muweke mambo sawa, muendelee kama zamani, inakuwaje hapo?

UCHEBE: Ndiyo maana nikakwambia mimi siku zote ni wa heri na sio wa shari hata kidogo, uelewe hivyo.

WIKIENDA: Nakushukuru sana Uchebe.

UCHEBE: Asante sana!

 

TUJIKUMBUSHE

Wawili hao walifunga ndoa kabla ya hivi karibuni Shilole kuibuka kwenye ukurasa wake wa Instagram na kutangaza kuachana naye, akidai kuwa amechoka kupigwa na mumewe huyo.

 

Shilole aliambatanisha na picha zilizoonesha amepigwa na kuzua huzuni kwa watu wengi, lakini hata hivyo baadaye ilielezwa kuwa picha hizo ni za zamani.

Stori: IMELDA MTEMA , Dar

Leave A Reply