The House of Favourite Newspapers

Uchumi Wetu Kiboko, SADC Yaimwagia Tanzania Sifa – Video

KATIBU Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)  Dk. Stergomena Lawrence Tax,  ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kuanza kwa mkutano wa SADC unaofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo, wakiwemo viongozi wastaafu na mawaziri, wamehudhuria.

Dk. Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo, pamoja na mambo mengine, kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama, na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakua kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.

“Uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekidhi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonesha Tanzania inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia saba, hivyo mjipongeze.

“Katika kufikia uchumi wa viwanda, nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda.  Nashukuru katika wiki ya viwanda iliyopita hivi karibuni, tumeshuhudia kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi wake unaendelea,” alisema.

FUATILIA MKUTANO HUO HAPA

YOU MAY LIK

Comments are closed.